MTEMBEZA wageni katika msitu wa hifadhi ya Ngezi
Makangale Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kusini Pemba, Mohamed Khalfan Massoud
akitoa historia ya Msitu huo, kwa wanafunzi wa skuli ya Sekondari Madungu Chake
Chake Pemba, wakati walipofanya ziara ya kitalii katika msitu huo wakiongozwa na Kamisheni ya Utalii Pemba.(Picha na
Abdi Suleiman, PEMBA).
WANAFUNZI wa Skuli ya Sekondari Madungu Chake Chake
Pemba, wakimsikiliza mtembeza wageni katika msitu wa Ngezi Makangale Mohamed
Khalfan Massoud, wakati alipokuwa akiwafahamisha aina za misitu iliyomo ndani
ya Msitu huo.(Picha na Abdi Suleiman,
PEMBA).
MTEMBEZA wageni katika msitu wa Hifadhi wa Ngezi
Makangale Mohamed Khalfan Massoud, akiwaonyesha wanafunzi wa skuli ya Sekondari
Madungu mabaki ya viwanda vya kupasualia mbao, kilichokuwa kikifanya kazi ndani
ya msitu wa ngezi katika kipindi cha wakoloni.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA).
MMOJA wa ina ya ndege adimu Zanzibar anayejulikana
kwa jina la Kidonati, ndege huyu
anadaiwa kutoa nchini Madagaska na hupatikana katika msitu wa ngezi Kisiwani
Pemba katika mwezi wa Septemba na Januari.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA).
MWANDISHI wa Habari wa ZBC TV kisiwani Pemba, Nassra
Mohamed Khatib akichukuwa baadhi ya maelezo ya mmoja wa ndege adimu
anayepatikana katika msitu wa ngezi Kisiwani Pemba, Kidonati ndege huyo anadaiwa kutoka nchini Madagaska.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA).
No comments:
Post a Comment