Habari za Punde

Balozi Seif Ali Iddi Ameondoka leo Mchana Kwenda India.na Safari ya Kikazi Nchini Ras Al Khaimah.

 
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Mgeni Juma Hassan akimsindikiza Balozi Seif  kuelekea Nchini India kupitia Mjini Dar es salaam kwa uchunguzi wa kawaida wa Afya yake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiagwa na Mkuu wa Wilaya ya  Mjini Nd. Maria Joel Thomas kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar  akielekea Nchini India kwa Uchunguzi wa Kawaida wa Afya yake.
Kati kati yao ni Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Mgeni Juma Hassan na nyuma ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi.
                                                   (Picha na – OMPR – ZNZ)

Na Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameondoka Zanzibar mchana huu kuelekea Nchini India Kupitia Mjini Dar es salaam kwa ajili ya uchunguzi wa kawaida wa Afya yake.

Balozi Seif anatarajiwa kuweko Nchini India kwa kwa muda mfupi na baadaye kupitia Nchini Ras Al -Khaimah kwa mapumziko mafupi pamoja na kufanya shughuli za Kiserikali na Viongozi wa Mamlaka hiyo kabla ya kurejea nyumbani Zanzibar kuendelea na uwajibikaji wa majukumu yake ya Kitaifa kama kawaida.

Katika safari hiyo Balozi Seif amefuatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi baada ya kuongoza mapokezi ya mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi aliyefariki Dunia Nyumbani kwake 
Mji Mwema Mjini Dar es  salaam na baadaye kwenda kutoa mkono wa pole kwa Familia ya marehemu Nyumbani kwake Migombani Mjini Zanzibar.

Kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Balozi Seif na Mkewe waliagwa na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Nd. Marina Joel Thomas akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohammed Mahmoud.

Wengine ni  Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi  Zanzibar Mh. Mgeni Juma Hassan , Viongozi Waandamizi wa Serikali, Kisiasa pamoja na Wakurugenzi na Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.