Mhe. Dkt. Mahadhi J. Maalim,
akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Ali Al-Yoha, Katibu
Mkuu, Baraza la Taifa la Sanaa na Utamaduni la Kuwait.
Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim,, amemtembelea Mhe. Ali
Al-Yoha, Katibu Mkuu wa Baraza la
Sanaa na Utamaduni la Kuwait ofisini kwake tarehe 04 Septemba 2016.
Katika ziara hiyo, Mhe. Dkt. Maalim alipata
fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Al-Yoha kuhusu masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya Tanzania na Kuwait katika eneo la Sanaa na Utamaduni. Mhe.
Al-Yoha, alimhakikishia Mhe. Maalim kuwa Kuwait ipo tayari kufanikisha ushiriki
wa Tanzania katika matamasha mbalimbali ya Sanaa na Utamaduni yanayoandaliwa na
Baraza hilo.
Kwa upande wake, Mhe. Dkt. Maalim, alimshukuru Katibu
Mkuu huyo na kumuahidi kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini Kuwait upo tayari kuratibu
zoezi hilo la upatikanaji wa vikundi vya utamaduni na sanaa kutoka Tanzania ili
viweze kushiriki katika matamasha hayo kwa lengo la kutangaza utamaduni na
sanaa ya Tanzania.
Kadhalika, Mhe. Maalim alisisitiza kuwa pamoja
na mambo mengine, eneo hilo la Sanaa na Utamaduni ni muhimu sana katika kukuza
mahusiano na maelewano ya watu wa pande hizi mbili.
No comments:
Post a Comment