Habari za Punde

Rais DK Shein ziarani Pemba

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wakati alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba leo  akitokea Unguja kwa ziara kikazi kisiwani humo akiwa na ujumbe aliofuatana nao akiwemo Mama Mwanamwemma Shein,[Picha na Ikulu.] 10/09/2016.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na MkeweMama Mwanamwema Shein wakisalimiana na Viongozi mbali mbali wakati walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Karume Pemba leo  kwa ziara maalum kisiwani humo,[Picha na Ikulu.] 10/09/2016.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kamanda wa KMKM Pemba wakati alipofika katika kituo kikuu cha karafuu cha ZSTC Wete Pemba kuangalia karafuu zilizokamatwa katika Bandari ya Tondooni  Mkumbuu Wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba,alipofanya ziara maalum leo,(wa pili kulia) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Bi.Amina Salum Ali, [Picha na Ikulu.] 10/09/2016. 

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mdhamini wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Nd,Abdalla Ali Ussi (kushoto) alipotembelea kituo kikuu cha karafuu cha ZSTC Wete Pemba kuangalia karafuu zilizokamatwa katika Bandari ya Tondooni  Mkumbuu Wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba leo alipofanya ziara maalum, [Picha na Ikulu.] 10/09/2016.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Bi.Amina Salum Ali (katikati) wakati alipotembelea kituo kikuu cha karafuu cha ZSTC Wete Pemba baada ya kuangalia karafuu zilizokamatwa katika Bandari ya Tondooni  Mkumbuu Wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba,akiwa katika ziara ya kikazi kisiwani humo,(kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Nd,Bakari Haji Bakari, [Picha na Ikulu.] 10/09/2016. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma (wa pili kushoto) wakati alipotembelea Uwanja wa Mpira wa Gombani kuangalia matengenezo makubwa yaliyomalizika kwa utiaji wa (Tatan) ambapo sasa Uwanja huo utaweza kutumika kwa shuhuli mbali mbali za michezo ikiwemo Riadha,(kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu), [Picha na Ikulu.] 10/09/2016. 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma (katikati) pamoja na Viongozi wengine  wakati alipotembelea Uwanja wa Mpira wa Gombani kuangalia matengenezo makubwa yaliyomalizika kwa utiaji wa (Tatan) ambapo sasa Uwanja huo utaweza kutumika kwa shuhuli mbali mbali za michezo ikiwemo Riadha, [Picha na Ikulu.] 10/09/2016.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.