Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein , Atuma Salamu za Rambirambi kwa Wananchi wa Mkoa wa Bukoba.

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
 Pemba                                                                   11.9.2016

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo na maafa mengine vilivyotokana na tetemeko la ardhi lililotokea jana Septemba 10, 2016 majira ya laasiri katika Mkoa wa Kagera pamoja na maeneo mengine ya jirani.

Kufuatia tukio hilo Rais wa Zanzibar anaungana na familia zote zilizopoteza ndugu, jamaa na marafiki na anawaombea marehemu wapumzishwe mahala pema  panapostahiki na awape subira ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu hao katika kipindi hiki kigumu.

Aidha, Dk. Shein amewaombea kwa Mwenyezi Mungu majeruhi wote walioathirika kutokana na tetemeko hilo wapone haraka na kurejea katika hali zao za kawaida ili waweze kufanya shughuli zao za kila siku kwa manufaa yao na taifa kwa jumla.

Wananchi wa Zanzibar wanaungana Mkuu wa  Mkoa wa Kagera, wananchi wake pamoja na Watanzania wote kwa jumla katika kuomboleza msiba huo.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.