WAZIRI wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji
Zanzibar Mhe:Balozi Ali Abeid Karume, akikagua barabara ya Ole-Kengeja eneo la
Mfikiwa,eneo ambalo udongo wake umelazimika kutolewa na kufukiwa fusi kulia ni
Injinia Amini Khalid Abdalla anaesimamia barabara hiyo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
AFISA Mdhamini Wilara za Ujenzi Mawasiliano na
Usafirishaji Pemba, Hamad Ahmed Mohamed (Baucha) kushoto akimpatia maelezo
Waziri wa Wizara hiyo Mhe:Balozi Ali Abeid Karume, wakati wa ziara yake ya
kukagua barabara ya Ole-Kengeja Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAFANYAKAZI wa barabara ya Ole-Kengeja wakiwa katika
kuchukua taarifa mbali mbali baada ya kukalisha vipimo vyao, kama walivyokutwa
wakipima baraabra hiyo katika eneo la Vitongoji.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAZIRI wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na
Usafirishaji Zanzibar, Mhe:Balozi Ali Abeid Karume, akimuelezea jambo Injinia
Mkaazi wa Wizara yake Pemba, Rashid Said wakati waziri huyo alipokuwa akikagua
barabara ya Mgagadu-Kiwani ambayo kwa sasa iko katika kiwango cha Lami.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAZIRI wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na
Usafirishaji Zanzibar, Mhe:Balozi Ali Abeid Karume, akikagua ukumbi utakaoweza
kufanyika sala ya Eid el hajj, mwaka huu huko Mkanyageni Wilaya ya Mkoani
Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman,
PEMBA.)
WAZIRI wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na
Usafirishaji Zanzibar, Mhe:Ali Abeid Karume akipata maelezo ya Ukumbi utakaofanyika baraza la Eid llhaji mwaka huu, huko Mkanyageni Wilaya ya Mkoani,
kushoto ni injinia Vekaria Mvrji kutoka kampuni ya Rans Consultation LTD
Zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman,
PEMBA.)
AFISA Mdhamini Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na
Usafirishaji Pemba, Hamad Ahmed Mohamed (Baucha), akimpatia maelezo waziri wa
Wizara hiyo Mhe:Balozi Ali Abeid Karume, wakati alipotembelea kukagua eneo
litakalo fanyika swala ya Eid ll Haj mwaka huu huko bandarini Mkoani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAZIRI wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na
Usafirishaji Zanzibar, Mhe:Balozi Ali Abeid Karume akizungumza na Ali Omnar
Khamis mmoja wa wakaazi wa nyumba za Maendeleo Kengeja, wakati wa ziara yake ya
kuangalia maendeleo ya Nyumba hizo.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAZIRI wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na
Usafirishaji Zanzibar, Mhe:Balozi Ali Abeid Karume akiteremka chini baada ya
kukagua nyumba za maendeleo Kengeja Mkoani.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
BAADHI ya maeneo ya nyumba za maendeleo Kengeja
yakiwa katika hali mbaya kama yanavyoonekana katika picha, nyumba hizo
zilijengwa na Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Amani Karume kwa ajili
ya wananchi.(Picha na Abdi Suleiman,
PEMBA.)
WAZIRI wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na
Usafirishaji Zanzibar, Mhe:Balozi Ali Abeid Karume, akimfahamisha jambo Afisa
Mdhamini wa Wizara hiyo Pemba, Hamad Ahmed Mohamed Baucha wakati walipokuwa
wakikagua nyumba za maendeleo Kengeja Mkoani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
Maendeleo ni kusonga mbele, lakini hizo nyumba za maendeleo naona zinarudi nyuma
ReplyDelete