Na Salmin .J. Salmin Pemba.
Jamii imeshauriwa kuuthamini utalii wa ndani ikiwa ni njia moja wapo ya kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kuitambua historia ya nchi yao
Mdahamini wa kamisheni ya Utalii Pemba Maalim Suleiman Amour Suleiman amesema endapo jamii itakuwa na utamaduni wa kuyatembelea maeneo hayo itapata fursa ya kuelewa mambo mbalimbali ya kihistoria na kuyaenzi kama kivutio kwa wageni
Hayo ameyasema huko Ras Mkumbuu alipokuwa katika ziara ya kuyatembelea magofu hayo na kubuni mikakati itakayosaidia kuyalinda ili kutopoteza haiba yake.
Naye msimamizi wa magofu ya Mkumbuu Rashid Ali Said amesema mbali na changamoto wanazokabiliana nazo katika kuyahifadhi maeneo hayo kutokana na uharibifu wa kimazingira lakini ufahamu mdogo wa wananchi juu ya kuyaenzi magofu hayo bado unarejesha nyuma ustawi wa magofu hayo.
Amesema katika kuyatangaza magofu ya Mkumbuu kiutalii huwaalika wananchi na wanafunzi kutoka skuli mbalimbali kutembelea na kujifunza historia ya mambo ya kale.
Magofu hayo ya Ras Mkumbuu ambayo yamevumbuliwa tokea karne ya tisa yamekuwa kivutizi kikuu cha utalii kutokana na historia yake ya kuwa na msikiti wakale na kaburi la mwanamwari.
No comments:
Post a Comment