Habari za Punde

Waziri wa Elimu Zanzibar aipongeza Kuwait kwa Misaada yake Kukuza Elimu Zanzibar.

Na Mwandishi Wetu.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma ameisifu na kupongeza mchango wa Kuwait katika kusaidia Taasisi za Elimu Visiwani Zanzibar.

Amesema kuwa kuna miradi mingi tofauti ambayo inaweza kuwa muendelezo wa ushirikiano na Nchi ya Kuwait iwe katika sekta ya Umma au Binafsi.

Miongoni mwa miradi hiyo ni kufundisha Lugha ya Kiarabu, na kutoa nafasi za masomo ya Elimu ya juu kwa wananfunzi wa Zanzibar katika taaluma ya sayansi, teknolojia, mafuta, uhandisi, dawa na lugha ya Kiarabu na masomo ya Kiislamu.

Mhe. Riziki pia amegusia misaada inayotolewa na Tasisi za Kuwait katika sekta ya Elimu kwa ujumla kama vile kujenga au kukarabati majengo ya skuli pamoja na kuwasaidia wazazi kugharamia elimu kwa idadi kubwa ya wanafunzi na kuwawezesha kuendelea na masomo yao.

Mhe.Riziki alitolea mfano wa Asasi ya African Muslim Agency Tawi la Zanzibar ilioko chini ya Tasisi ya  Direct Aid amabyo inatoa nafasi za masomo ya Sekondari kwa watoto wa Kike wa Zanzibar katika skuli ya Ihsan,ilioko mwanakwerekwe ijitimai ya zamani, na kutoa nafasi za masomo ya Elimu katika Chuo kikuu cha Dr.Abdul Rahman Al Sumait ambacho kimekuwa na mchango mkubwa katika kujenga Mustakabali mzuri kwa vijana wa Kizanzibari katika kupambana na changamoto mbali mbali na kutumikia jamii zao kwa njia nzuri  Zaidi.

Kwa upande wake, Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasim Al Najem ameleza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuzisaidia taasisi za elimu Zanzibar, na kwamba ushirikiano wa pamoja na Wizara ya Elimu ya Kuwait inaweza kuwa mwanzo wa ushirikiano wa karibu wenye manufaa zaidi.

Mhe. Al- Najem ameongeza kuwa kusaini kwa makubaliano baina ya Chuo Kikuu cha Kuwait na Vyuo Vikuu Vya Tanzania, ikiwa ni pamoja Vyuo Vikuu vya Zanzibar itakuwa ni hatua kubwa katika kujenga ushirikiano katika sekta ya elimu na utamaduni na kutawezesha pande hizo mbili kutoa nafasi za elimu na kubadilishana uzoefu baina ya walimu na utekelezaji wa mipango kadhaa ya kimaendeleo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.