Habari za Punde

Alloo avitaka vyombo vya habari kusaidia kulaani vitendo vya ubakaji

 Wanafunzi kutoka shule ya mandalizi ya Madrasatul Nasril Islamiyya ya mjini Zanzibar wakisoma utenzi mbele ya mgeni rasmi, Yasmin Alloo jana.Kutoka kushoto ni Hajra Suleiman, Asia Mharami na Hairat Hamad
Picha na Martin Kabemba.
 Yasmin Alloo akizungumza kwenye sherehe hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya mandalizi ya Kidutani mjini Zanzibar.
Picha na Martin Kabemba

Mjumbe wa zamani wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Yasmin Alloo amevitaka vyombo vya habari nchini kusaidia katika mapambano na kulaani vitendo viovu wanavyofanyiwa watoto vikiwepo ubakaji na utumikishwaji wa ajira zisizo rasmi.

Akizungumza kwenye sherehe za wazazi wa shule ya mandalizi ya Madrasatul Nasril Islamiyya ya mjini Zanzibar jana, akiwa mgeni rasmi, Yasmin pia amewataka wazazi kufufua utamaduni wa kizanzibari katika malezi ya watoto kwa kufuata maadili ya kizanzibari badala ya kuwaacha wakiiga tamaduni za mataifa ya kigeni,

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.