Habari za Punde

Kama Matangazo Hamna Basi Tuige Mfano Huu Uwanjani Kwetu Kuvutia Uwanja.

Viwanja vingi sana vya michezo duniani hasa vile vya mpira wa miguu huonekana kupambwa na mabango mengi ya matangazo nje na ndani husu yale ya wadhamini wa mchezo husika.


Kuna yale ambayo huwekwa pembezoni mwa majukwaa ya watazamani na mengine hupita kwa mtindo wa kisasa(Electronics) kwenye eneo husika.
Miaka mitatu iliyopita viwanja vya Amaan na ule wa Gombani vilionekana kuwa na mabango hayo kupitia udhamini wa ligi kuu uliokuepo yaani Grand Malt.

Baada ya mdhamini huyo kuondoka hakuna tena mabango hayo. Lakini mtandao huu unakuja na ushauri juu ya mfano ulioanza kuonyeshwa na baadhi ya mashabiki wa timu.

Kiukweli nafsi yangu ilivutika sana kuona mashabiki wa timu ya Taifa ya Jang'ombe, Jang'ombe Boys na baadhi ya siku Kilimani City wakipamba majukwaa kupitia mabango yao.
Ikiwa hali kama hiyo hapo juu itaigwa na mashabiki wa timu nyengine naamini hata taswaira ya viwanja vyetu itapendeza na itakua chachu ya kuwavutia wawekezaji na makampuni kusogea kwenye ligi yetu kwa lengo la udhamini.

Waswahili wanasema "Kuiga jambo jema si vibaya".
Kwanini basi mashabiki wa timu husika washindwe kufanya hivyo.
Kumbuka mjenga nchi ni mwananchi, na mvunja nchi ni mwananchi. Kama matangazo hamna basi tuupambe uwanja kwa mabango ya mashabiki.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.