Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk Shein Atembelea Ujenzi wa Barabara Kisiwani Pemba, Akiwa Katika Ziara yake Kisiwani Humo.

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi dk: Ali Mohamed Shein, akisalimiana na viongozi  kadhaa wakati alipowasili kwenye shehia ya Minazini wilaya ya Mkoani Pemba, kwa ajili ya kuikagua barabara ya Mgagadu –Kiwani, ikiwa ni sehemu ya izaya yake ya siku tatu kisiwani  humo
  MKURUGENZI wa Idara ua Ujenzi na Utunzaji wa Barabara UUB Zanzibar Ali Tahir Fatawi, akimuelezea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi dk: Ali Mohamed Shein, juu ya ujenzi na changamoto za barabara ya Mgagadu- Kiwani wilaya ya Mkoani Pemba,
 WANANCHI wa shehia ya Minazini wilaya ya Mkoani Pemba, waliofika kwenye eneo la barabara hiyo, kwa ajili ya kusalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi dk: Ali Mohamed, wakati alipoitembelea barabara yao ya Mgagadu- Kiwani

 MWANANCHI wa Kiwani Abdalla Makame Hamad, akimueleza jambo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi dk: Ali Mohamed, wakati alipoitembelea barabara yao ya Mgagadu- Kiwani, na kutoa nafasi kwa wananchi kusema chochote
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wananchi wa Mgagadu -Kiwani wakati alipofika kuangalia maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo.

MWANANCHI wa Kiwani Abdalla Makame Hamad, akimueleza jambo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk: Ali Mohamed, wakati alipoitembelea barabara yao ya Mgagadu- Kiwani, na kutoa nafasi kwa wananchi kusema chochote

SHEHA wa shehia ya Kendwa wilaya ya Mkoani Pemba, Sabiha Mohamed Ali akiuliza suali kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk: Ali Mohamed, wakati alipoitembelea barabara yao ya Mgagadu- Kiwani,
AFISA Mdhamini wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Pemba, Juma Bakar Alawi akitoa ufafanuzi wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa shehia ya Minazini Wilaya ya Mkoani, baada ya wananchi hao kumueleza rais usumbufu wa huduma hiyo, wakati alipoitembelea barabara ya Mgagadu –Kiwani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed, akiangalia moja ya madaraja yaliomo kwenye barabara ya Mgagadu- Kiwani, mara baada ya kupata maelezo ya ujenzi wa kiwango cha lami barabara hiyo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.