Habari za Punde

Rais Dk Shein alipojumuika na viongozi, wanajeshi na wanafamilia kuuaga mwili wa Brigadier General Mhaiki

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK ALI MOHAMED SHEIN AMEWAONGOZA VIONGOZI,WAKUU WA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA PAMOJA NA WANAFAMILIA KUUAGA MWILI WA BREGEDIA JENERAL CYRIL IVORY MHAIKI,KAMANDA WA BRIGEDI YA NYUKI ZANZIBAR,ALIYEFARIKI DUNIA TAREHE 13 DEC 2016 KATIKA HOSPITAL YA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA,LUGALO DAR ES SALAAM. MWILI WA MAREHEMU BRIGEDIA JENERAL CYRIL MHAIKI UMEAGWA AMBAPO DK SHEIN ALIFIKA HOSPITAL YA LUGALOMAJIRA YA SAA NNE ASUBUHI AKITOKEA ZANZIBAR AKIWA AMEONGOZANA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR WAKIWEMO MAWAZIRI NA WATENDAJI WENGINE WA SERIKALI.


 
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Dar-es-Salaam                            16.12.2016
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amewaongoza viongozi, wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama pamoja na wanafamilia kuuaga mwili wa Marehemu Bregedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki, Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar,aliyefariki dunia tarehe 13, Disemba 2016 katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzaia, Lugalo Dar-es-Salaam.

Mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki umeagwa leo huko katika Hospitali ya Jeshi la Wananachi wa Tanzania, Lugalo jijini Dar-es-Salaam ambapo Dk. Shein alifika Hospitalini hapo, majira ya saa nne za asubuhi akitokea Zanzibar akiwa ameongozana na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwemo Mawaziri na Watendaji wengine wa Serikali.

Akiwa Lugalo Dk. Shein alipokewa na viongozi mbali mbali wakiongozwa na Waziri wa Ulinzi  na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussen Mwinyi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Adolf Mwamunyange, viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Viongozi wengine wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama ambapo Dk. Shein aliaanza kwa kutia saini kitabu cha maombolezo.

Katika tukio hilo ambapo baadhi viongozi wakuu wa Jeshi wastaafu walihudhuria, Dk. Shein aliongoza waombolezaji kutoa salamu za mwisho, ambapo salamu mbali mbali zilitolewa kutoka kwa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na makundi maalum.

Katika salamu za rambi rambi zilizotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekitiwa Baraza la Mapinduzi ambazo  zilisomwa na Bregedia Jenerali Kayombo zilieleza namna Dk. Shein, pamoja na wananchi wote wa Zanzibar walivyopokea kwa mshtuko taarifa ya kifo cha Kamanda huyo hodari, aliyetoa mchango mkubwa katika shughuli za ulinzi na usalama na maendeleo ya Tanzania kwa jumla.

Salamu hizo zilieleza namna Marehemu Mhaiki alivyokuwa mtu mwenye mashirikiano na wenziwe, muadilifu, msikivu na Kamanda mahiri katika kazi zake.

Salamu nyengine mbali mbali za rambi rambi zilitolewa zikiwemo salamu kutoka Baraza la Michezo ya Majeshi  Tanzania (BAMATA) ambalo Marehemu alikuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo, salamu ambazo zilieleza namna alivyokuwa mstari wa mbele katika kuimarisha na kuiendeleza michezo ya Majeshi na hatimae kupata mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi.

Aidha, salamu hizo zilieleza kuwa Jenerali Mhaiki atakubukwa katika mchakato wa kurejesha mashindano katika kikosi hicho na tangu kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa BAMATA mnamo Septemba, 24 mwaka 2013 mafanikio makubwa yameweza kupatikana na kuahidi kuyafuata mazuri yote aliyoyaacha.

Akitoa neno la shukurani kaka wa Marehemu Oliva Mhaiki, alimsukuru Rais wa Zanzibar nan Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein kwa kwenda kuungana nao katika kuuaga mwili wa mdogo wake pamoja na viongozi wote aliohudhuria katika tukio hilo.

Brigedi ya Nyuki Zanzibar nayo ilitoa salamu zake za rambi rambi kwa kifo cha Bregedia wake Jenerali Cyril Ivor Mhaiki na kusisitiza kuwa ameacha pengo kubwa kwa Brigedi hiyo, familia pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na nchi kwa jumla sambamba na kukumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika malezi ya askari.

Kaka huyo wa Marehemu alitumia fursa hiyo kutoa shukurani kwa madaktari wa hospitali hapo kwa kumuuguza marehemu pamoja na kutoa shukurani kwa Jeshi la Ulinzi Tanzania kwa kutoa huduma kwa ndugu yake.

Mwili wa marehemu umesafirishwa leo kutoka Hospitalini hapo kuelekea  Songea Mkoani Ruvuma ambako mazishi ya Jenerali Mhaiki yatafanyika siku ya Jumaapili  Disemba 18, mwaka huu sambamba na taratibu zote za kijeshi, ambapo pia, salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Johm Pombe Magufuli zitatolewa katika mazishi hayo.

Marehemu Mhaiki amezaliwa Disemba 16 mwaka 1954 huko Mbinga Ruvuma na kupata elimu ya Msingi na Sekondari katika skuli na vyuo tofauti ambapo alijiunga na Jeshi mnamo mwaka 1973 na kupata Kamisheni mwaka uliofuata na kupita ngazi tofauti na hatimae kupandishwa vyeo na kufikia Bregedia Jenerali hadi kufariki kwake.

Sambamba na hayo, Jenerali Mhaiki alitunukiwa medali mbali mbali kutokana na uongozi wake mahiri. Marehemu Mhaiki ameacha Mjane na mtoto mmoja.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.