Habari za Punde

Unesco: Tupo tayari kwa mashirikiano kuhakikisha kuhakikisha watoto wanapata elimu inayokubalika

Na Kailani Juma, Pemba

Shirika la kimataifa la elimu , sayansi ,utamaduni na habari la umoja wa mataifa UNESCO limesema liko tayari kushirikiana na wadau mbali mbali wa elimu nchini Tanzania kusaidia kutatua changamoto zinazo ikabili sekta ya elimu ilikuengeza ubora wa elimu nchini.

Kauli hiyo imetolewa na katibu mtendaji wa UNESCO nchini TANZANIA dk Moshi Mussa Kimizi alipokuwa akizungumza na walimu wa shule mbali mbali kisiwani Pemba kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Fedel Castro Chakechake Pemba.
Amesema UNESECO iko tayari kuhakikisha elimu inabaki kuwa haki ya kila mtoto kuipata na kuwa ngao ya kuchochea maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake afisa mdhamini Wizara ya elimu na mafunzo ya amali Pemba Salimu Kitwana Sururu amewataka walimu kuacha kufundisha kwa mazoea badala yake watumie mbinu na ubunifu ilikufanikisha kuleta mageuzi ya ufaulu mkubwa kwa wanafunzi ktika mtihani yao ya taifa

Nae mkuu wa sekta ya elimu tume ya taifa bi Fatma Shabaan Mpore amesema wanafunzi kushirikishwa katika majaribio na mitihani ya darasani kutawajenga kuwa na uwezo wa kujiamini katika ngazi za elimu mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.