Habari za Punde

ZIRPP Monthly Lecture: Kunyanyuka na Kuanguka kwa Maendeleo ya Michezo Zanzibar

Chairperson: Dr. Ahmed Gurnah
Speaker: Mr. Seif Nassor Mshumaa
Subject: "Kunyanyuka na Kuanguka kwa Maendeleo ya Michezo Zanzibar" (Rise and Fall of the Development of Sports in Zanzibar

Date & Time: Saturday 31 December 2016; at 4:00 pm.
Venue: ZIRPP Office,Third Floor, behind Majestic Cinema (above ZANLINK
ABSTRACT: Kwa muda mrefu, michezo mbali mbali, ambayo imechangia sana katika kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar na kuwaleta pamoja, na kuimarisha afya na siha zao, imekuwa ikiendelezwa nchini Zanzibar kwa ari, kasi na mafanikio makubwa. Michezo hii ni pamoja na mpira wa miguu, hokey, cricket, lawn tennis, table tennis, badminton, volleyball, swimming, golf, resi za ngalawa, resi za baiskeli, riadha na kadhalika. Katika miaka ya 1940 hadi 1970s, Zanzibar imeweza kupata sifa kubwa katika michezo mbali mbali ndani na nje ya nchi, na Serikali na Wazanzibari kwa jumla wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika kuikuza na kuiendeleza michezo hii nchini.
Kwa mfano, mpira wa miguu ni mchezo mmoja uliokuwa ukipendwa sana na Wazanzibari wengi hasa baada ya Timu ya Zanzibar kulitwaa Kombe la ushindi katika mashindano ya Kombe la Chalenji linalojumuisha Timu mbali mbali kutoka nchi za Afrika ya Mashariki.  Lakini, kwa bahati mbaya, hali ya michezo imeanguka sana kiasi cha kuwafanya Wazanzibari kuhusudu na kushabikia timu za mpira wa miguu za Uingereza, Hispania, Italy na Ujarumani zaidi kuliko timu za hapa kwetu.  Isitoshe, kiwango cha michezo ya riadha nacho kimeanguka sana; na hivyo hivyo ndivyo ilivyo kuhusiana na michezo mengine yote.
Katika kujadili kisa na sababu za kuanguka kwa kiwango cha michezo nchini Zanzibar, mwanamichezo maarufu, Seif Nassor Mshumaa, akishirikiana na wanamichezo wengine mashuhuri wa Zanzibar, atalijadili suala hili kwa kina kwa madhumuni ya kuzingatia wapi tulipoangukia na jinsi ambavyo Zanzibar itaweza kunyanyuka tena na kufanya vizuri zaidi katika jitihada za kuhuisha na kuinua viwango vya michezo mbali mbali hapa nchini.
Tea, Coffee and Snacks will be served freely.
Please forward this message to anybody who may be interested. Those who would like to attend should send their email addresses and telephone numbers to: zirpp@googlegroups.com.
Please confirm your participation. You may bring one or two friends with you.
All are welcome.
Muhammad Yussuf
Executive Director
Zanzibar Institute for Research and Public Policy
P.O. Box 4523, Zanzibar, Tanzania;
Tel: +255 242 223-8474;
Fax: +255 242 223-8475;
Cellular: 0777 707820;
Website: www.zirpp.info

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.