Habari za Punde

Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Ndg Mpogoro Azindua Matembezi ya Vijana wa UVCCM, Donge Zanzibar leo.

Viongozi wa UVCCM Tanzania wakiwa na Mlezi wa UVCCM Mama Asha Suleiman wakiaza matembezi hayo ya Vijana wa CCM yalioazia katika viwanja vya mpira Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja na kuelekea katika kituo cha kwanza cha matembezi hayo katika viwanja vya Machuwi Wilaya ya Kati Unguja kwa mapumziko na kuaza matembezin hayo kesho na kumalizia katika viwanja vya maisara.  
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Vijana wakati wa uzinduzi wa Matembeza ya Vijana ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliozinduliwa katika viwanja vya donge Wilaya ya Kaskazini B Unguja, na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Bara Ndg Rodrick Mpogoro.
Viwanaja wanaoshiriki matembezi ya kuwaenzi Wanamapinduzi ya Zanzibar wakiwa katika viwanja vya hafla hiyo katika kijiji cha donge Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na Mbunge wa Jimbo la Donge Mhe Sadifa, akizungumza wakati wa hafla hiyo na kuwatambulisha wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa matembezi hayo 
Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja Ndg Issa Juma Ali akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa matembezi kwa Vijana wa UVCCM uliofanyika katika viwanja vya mpira donge Zanzibar. MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarb Mama Asha Suleiman Iddi, akikabidhi msaada wa vyakula kwa ajili ya Vijana wanaoshiriki matembezi kwa Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Bara. Ndg Rodrick Mpogoro, wakati wa hafla ya kuzindua matembezi hayo yalioazia katika viwanja vya mpira donge Mkoa wa Kaskazini Unguja
NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Bara Ndg. Rodrick Mpogoro, kulia akimkabidhi mifuko 100 ya saruji Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja Ndg.Issa Juma Ali kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Donge, saruji hiyo imetolewa na Umoja wa Vijana Tanzania hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya mpira donge

NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg Rodrick Mpogoro akiwahutumia vijana 400 wanaoshiriki matembezi ya Vijana wa UVCCM ikiwa ni shamrashara za kusherehea miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yalioazia katika viwanja vya mpira donge wilaya ya kaskazini B unguja

VIJANA wa Umoja wa Vijana wa CCM wakimshangilia Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM wakati wa uzinduzi wa matembezi hayo yaliowashirikisha vijana 400 kutoka Zanzibar na Tanzania Bara. Yalioazia katika viwanja vya mpira donge Wilaya ya Kaskazini B UngujaNo comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.