Naibu Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana
maafisa wa Jeshi la Polisi baada ya kuwasili mkoani Songwe kwa ziara ya kikazi
na kutembelea idara zilizopo chini ya wizara yake kwa lengo la kufuatilia
utendaji kazi wa idara hizo na kuzishauri
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Mathias
Nyange(kulia), akimuongoza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni kutembelea makao makuu ya Jeshi la Polisi mkoani Songwe wakati wa
ziara ya naibu waziri yenye lengo la kufuatilia utendaji kazi wa idara za
wizara yake na kuzishauri ili kuweza
kudhibiti hali ya uhalifu mkoani hapo
Naibu Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na
wakuu wa Idara zilizopo chini ya wizara yake, alipowasili mkoani Songwe kwa
ziara ya kikazi ikiwepo kufuatilia utendaji wa idara hizo katika kukabiliana na
hali ya usalama kwa mikoa iliyopo mipakani
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa
Idara ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Mkoa wa Songwe, Coletha Peter,
alipofanya ziara katika ofisi hizo kwa lengo la kujua zoezi la kuandikisha
wafanyakazi wa umma lilipofikia
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni,
akizungumza baada ya kupata maelezo ya
mradi wa Ujenzi wa ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe unaojengwa kwa
ushrikiano wa wadau wa mkoa huo na jeshi la polisi.Wapili kushoto ni Kamanda wa
Polisi wa mkoa huo ACP Mathias Nyange
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad
Masauni(watano kulia), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa idara
zilizopo chini ya wizara yake katika mkoa wa Songwe mara baada ya kufanya mazungumzo na wafungwa
katika gereza la wilaya ya Mbozi ambapo aliwataka kufanya kazi wanazopangiwa
ili wawe rasilimali watu katika dhana ya kulipeleka Taifa katika uchumi wa
kati
.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI –WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment