Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala, katika Sherehe za Kukabidhi Bima ya Afya kwa Wazee wa Jimbo
la Kikwajuni, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnarani, MwembeKisonge, MjiniUnguja,
Zanzibar.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kikwajuni
(hawapopichani), kabla ya kukabidhi kadi za Bima ya Afya kwa wazee zaidi ya 200
wa jimbo hilo ambalo anatoka Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad
Masauni (kushoto). Kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo,Mhe. Nassor Salim Jazeera.
Tukio hilo lilifanyika katika Viwanja vya Mnarani, MwembeKisonge, Mjini Unguja,
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala, akimkabidhi Bi. Salma
Salum kadi ya bima ya Afya katika viwanja vya Mnara wa Michezani MwembeKisonge, Mjini Unguja,
Zanzibar. Kadi zaidi ya 200 walikabidhiwa wazee wa Jimbo la
Kikwajuni la Mhe Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wananchi wakati wa hafa hiyo ya kukabidhi Kadi za Bima ya Afya kwa Wazee wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar jumla ya wazee 200 wamefaidia na mchango huo wa Mbunge na Mwakilishi kupata matibabu bure kwa kutumia kadi hizo. Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya mnara wa kumbukumbu michezani kisonge.
Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapindiuzi,
Zanzibar, Mhe.Harusi Said akizungumza na wananchi katika Sherehe za kukabidhi Bima ya Afya kwa Wazee zaidi ya
200 wa Jimbo la Kikwajuni, zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Mnara wa Michezani Zanzibar. MwembeKisonge, MjiniUnguja, Zanzibar. Pichana
Felix Mwagara.
No comments:
Post a Comment