Habari za Punde

Tamasha la Muziki Kusherehekea Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar Katika Viwanja vya Maisara Zanzibar Mkesha wa Fashfash.

 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mahmuod Mohammed akizungumza na Wananchi katika viwanja vya maisara Zanzibar wakati wa Tamasha la Mkesha wa kusherehekea miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa kupigwa kwa fashfashi katika viwanja hivyo. Tanmasha hilo limetayarishwa na G 1 na wasanii wa Zanzibar wa muziki wa Zenj Flava.

Mratibu wa maandalizi ya upigaji wa fashfashi kwa niaba ya Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said na Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni Mhe Husein Ibrahim Makungu  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayuob Mohammed Mahmoud akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Tamashala la Mkesha la Muziki wa Zenj Flava lililofanyika katika viwanja vya maisara ikiwa ni kusherehekea miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.  
Mratibu wa Tamasha la Muziki wa Kizazi Kipya Zanzibar na Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni Zanzibar Mhe Hussein Ibrahim Makungu BHAA akitowa maelekezo wakati waTamasha hilo la Mkesha wa kusubiri fashfashi kusherehekea miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar  lililofanyika katika viwanja vya mpira maisara usiku wa tarehe 11-1-2017 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.