Habari za Punde

Jaji Mkuu azindua mahakama ya mwanzo Wilaya ya Micheweni

Na Salmin Juma, Pemba

Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu ameizindua Mahkama ya mwanzo ya Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni ikiwa ni katika  maadhimisho ya wiki ya siku ya Sheria Zanzibar.

Katika hutuba yake ya uzindunzi wa Mahkama hiyo iliyosomwa na Mrajisi wa Jimbo Hossein Makame Hossein kwa niaba yake amesema Mahkama  hiyo itasaidia kuongeza mapato ya Halmashauri zitokanazo na faini kwa wale wanaokwenda kinyume na taratibu.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni Hamad Mbwana shehe amesema mahkama hiyo itakuwa huru na itatenda haki kwa wananchi na kuhakikisha wanatatua migogoro inayojitokeza.

Katika risala ya uzindunzi iliyosomwa na Rukia Khamis Said amesema Halmashauri inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ucheleweshwaji wa maamunzi ya kesi kutokana na uwepo wa kesi nyingi mahkamani.

Kwa upande wao baadhi ya wadau waliohudhuria uzindunzi huo wameelezea matumaini yao juu ya kuanzishwa kwa mahkama hiyo.

Siku ya sheria Zanzibar huadhimisha  kila ifikapo tarehe februari 11 kila mwaka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.