Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskzini Pemba, Haji Khamis Haji, akitowa maelezo ya kukamatwa kwa karafuu hizo ambazo zilikuwa zinataka kusafirishwa kwa magendo.
Gari za aina ya Noha na gari la Ng'ombe ambazo zilikamatwa zikiwa zimepakia Karafuu za magendo mkoa Kaskazini Pemba.
Picha na Hanifa Salim-Pemba.
NA/ HANIFA SALIM—PEMBA.
JUMLA ya magunia matano ya Karafuu kavu yenye uzito wa
kilo 300, yamekamatwa na vikosi vya Ulinzi na usalama katika maeneo ya
Chanjaani na kiperani Konde Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Magunia
mawili yalikamatwa Januari 4 yakiwa katika gari aina ya Noah yenye namba Z529GH
na matatu Febuari 8 mwaka huu yakiwa katika gari ya Ng’ombe ambayo yalikamatwa
na askari wa Vikosi vya ulinzi na usalama wakiwa katika doria majira ya saa
7:00 usiku.
Akizungumza
na mwandishi wa habari Mkurugenzi mwendeshaji wa Shirika la ZSTC Zanzibar, Said
Seif Mzee, aliwataka wananchi kuuza Karafuu ZSTC, alisema karafuu ni zao la nchi ambalo linamgusa kila Mzanzibar
hivyo wananchi wanapouza karafuu ZSTC inasaidia Serikali kuongeza mapato.
Alisema
Serikali imefanya juhudi ya kuwalipa
wananchi bei nzuri kwa mauzo ya zao la Karafuu ambayo bei hiyo haipatikani
katika nchi yoyote, hivyo ni vyema jamii iache kusafirisha karafuu kwa njia ya
magendo.
“Katika
kuziangalia karafuu hizi ambazo zimekamatwa zimeonekana kuwa vimechanganywa na
makonyo ambapo hii ni kutokana na kutaka waziongeze uzito njambo ambalo ni kosa
kisheria” alisema.
Hata
hivyo thamani ya Karafuu hizo , haikuweza kupatikana kwa vile hazijafanyiwa
upasishaji, na kutiwa bei yake halisi kulingana na ubora ilizonazo.
Alieleza
kwa mujibu wa sheria ya maendeleo ya Karafuu
ya mwaka 2014, Sheria namba mbili sehemu ya 19 kifungu cha kwanza hadi cha sita,
kimelezea usafirishaji wa karafuu kavu kutoka sehemu moja kwenda nyengine ni lazima
kupata kibali.
Alisema
Shirika linaendelea kushawishi wananchi
katika kuuza karafuu zao ZSTC na kuacha kusafirisha kimagendo jambo ambalo ni
makosa na linasababisha kupunguza pato la nchi.
Kamanda
msaidizi Kamishna wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji,
akithibitisha kukamatwa kwa magendo ya karafuu hizo alisema, ni kweli askari
walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao kwa siku tafauti wakiwa katika shughuli
zao za doria.
“Kuna
karafuu zilikamatwa na wenzetu wa KMKM Konde katika gari aina ya Noha ambapo mtuhumiwa
alikimbia, lakini asubuhi walikamatwa na Febuari 8 tulimkamata mtuhumiwa
mwenginea kutoka konde kwenda bandari ya Kichungwani Msuka na wote tutafikishwa
mahakamani Jumatatu” alisema.
Hivyo
aliwataka wananchi na wakulima wote wa zao la Karafuu watumie fursa ya kuuza Karafuu
zao ZSTC, ili kulipatia Shirika mapato halali ya nchi na kuacha kusafirisha Karafuu
kimagendo pia wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili wananchi waache
tabia hiyo.
No comments:
Post a Comment