Habari za Punde

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein Afungua Kongomano la Kupinga Unyanyasaji wwa Wanawake na Watoto Zanzibar.," Likiwa na Kauli Mbiu Unyanyasaji Kinamama na Watoto Sasa Basi "

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Mstaaf wa Mjini Magharibi Mhe Abdalla Mwinyi Khamis alipowasili katika viwanja vya Wizara ya Habari Zanzibar kwa ajili ya Ufunguzi wa Kongamano la Kupinga Vitendo vya Unyanyasaji wa Wanawake na Watoto Zanzibar lililoandaliwa na Taasisi ya Siti Bint Saad Zanzibar.
Mwanaharakati wa Siti Bint Saada akimvisha Beji ya Taasisi ya Siti Bint Saad Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein alipowasili katika viwanja hivyo.  
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mhe. Maudline Cyrus Castico wakielekea katika ukumbi wa mkutano.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa na Viongozi wa meza Kuu wakishangiliwa wakati wa kipokelewa katika ukumbi wa Mkutano kulia Mwenyekiti wa Taasisi ya Siti Bint Saad Bi Nasra Mohammed Hilal Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Mgeni Hassan Juma na Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Maudline Cyrus Castico.
Washiriki wa Kongamano hilo wakimpoea Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein alipowasili ukumbi wa Mkutano huo.
MC wa Kongamano hilo Bi Hasina Hamadi akitowa maelezo kabla ya kuaza kwa Kongamano hilo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Zanzibar. 
Wanafunzi wakisoma Utenzi wakati wa Mkotano wa Kongamano wa Kupinga Unyanyasaji wa Wanawake na Watoto Zanzibar.  
Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Maudline Cyrus Castico.akizungumza wakati wa Kongamano hilo. 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Siti Bint Saad Bi Nasra Mohammed Hilal akizungumza wakati wa Kongamano hilo na kutowa maelezo ya kusudio lake kupinga Vitendo vya Unyanyasaji wa Wanawake na Watoto Zanzibar.  
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akifungua Kongamano la Siku moja juu ya Vitengo vya Unyanyasaji wa Wanawake na Watoto Zanzibar, na kuvikemea vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi ya Watu kutumia uwezo wao.kuwadhalilisha Watoto na Wanawake Zanzibar.Kongamano hilo limeandaliwa na Taasisi ya Siti Bint Saad Zanzibar.  
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema akisisitija jambo wakati akifungua Kongamano hilo lililowashirikisha wadau mbalimbali wa sekta za Serikali na Binafsi.,
Washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia na kutowa nasaha zake kwa washiriki hao. 
Washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia na kutowa nasaha zake kwa washiriki hao. 
Mtoa Mada kutoa Dawati la Wanawake Rahma Ali akitowa Mada kuhusiana na Vitendo vya Unyanyasaji wa Wanawake katika Jamii 
Daktari kutoka Kituo cha Mkono kwa Mkono katika hospitali ya Mnazi Mmoja Dr. Fatma akitowa Mada katika Konngamano hilo jinsi wanavypokea kesi za uchunguzi wa vitendo vya Unyanyasaji wa Wanawake na Watoto wanaofika katika hospital hiyo kwa uchunguzi. 
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha SUZA Zanzibar Dk. Issa Ziddy akitowa mada wakati wa Kongamano hilo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani kikwajuni Zanzibar 
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia Mada zinazowasilishwa na Wahusika.
Mtoa Mada kutoka Jumuiya ya Maimamu Zanzibar Sheikh Nassor akitowa Mada kuhusiana na Tafiti walizofanya kutokana na vitendo vya unyanyasaji wa Watoto wadogo katika maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba. akiwasilisha Mada hiyo kwa washiriki wa Kongamano hilo. lililoandaliwa na Taasisi ya Siti Bint Saad Zanzibar kupiga vitendo vya Unyanyasaji wa Wanawake na Watoto Zanzibar.
Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia Mada zinazowakilishwa na Watoa Mada katika Kongamano hilo.
Baadhi ya Wanafunzi wa Skuli za Unguja wakiwa katika ukumbi wa Mkutano wakifuatilia mijadala na Mada zikiwakilishwa. 
Baadhi ya Wanafunzi wa Skuli za Unguja wakiwa katika ukumbi wa Mkutano wakifuatilia mijadala na Mada zikiwakilishwa. 
Washiriki wakichangia mada na kutowa ushauri jinsi ya kufanya kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji wa Wanawake na Watoto katika vitendo vya ulawiti vilivyoshamiri katika maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba kwa watoto wadogo wanaofanyiwa ukatili huo.




Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Wanaharakati wa Taaisi ya Siti Bint Saad , walioandaa Kongamano hilo la  Kupinga Unyanyasaji wa Wanawake na Watoto Zanzibar lililofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Zanzibar lililoandaliwa na Taasisi ya Siti Bint Saad. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi walioshiriki Kongamano la Kupinga Unyanyasaji wa Wanawake na Watoto Zanzibar lililofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Zanzibar lililoandaliwa na Taasisi ya Siti Bint Saad. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.