Habari za Punde

Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya Zantel - Zanzibar Wachangia Damu Kusaidia Benki ya Damu Salaama Nchini

 MKUU wa kampuni ya simu Zantel Zanzibar Mussa Khamis Mohammed ‘Baucha’, akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 28, 2017 kuhusu zoezi la kuchangia damu lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo kwenye makao makuu Amani mjini Unguja.
MFANYAKAZI wa benki ya damu Zanzibar (kushoto) akichukua maelezo kutoka kwa mmoja wa watendaji wa kampuni ya simu Zanzibar Zantel, kabla hajatolewa damu kuchangia akiba ya benki hiyo. Zoezi hilo limefanyika leo Februari 28 makao makuu ya Zantel Amani mjini Unguja.

Na Mwandishi Wetu

Katika kuisaidia benki ya damu hapa nchini, wafanyakazi wa Zantel-Zanzibar leo wamejitokeza kwa wingi na kujitolea kuchangia damu katika kuendeleza mwitikio huo kwa jamii ulioanzishwa na Kampuni hiyo wiki iliyopiata katika makao makuu yake jijini Dar es Salaam.

Zoezi hili ambalo linaratibiwa na Kitengo cha uwajibikaji kwa jamii (CSR) cha Kampuni hiyo, limelenga kusambaza upendokupitia shughuli hii ya uchangiaji damu ili kuiwezesha benki ya damu sambamba na kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu.

Shughuli hiyo ya uchangiaji iliyofanyika katika makao makuu ya Ofisi za Zantel-Zanzibar, ilishuhudia mwitikio mkubwa kutokana na wingi wa wafanyakazi wa Zantel kujitokeza, pamoja na baadhi ya wananchi wakishiriki kuchangia damu.

Akizungumza wakati wazoezi hilo la uchangiaji damu, Mkurugenzi wa Zantel Zanzibar, Bw. Mohamed Musa Baucha aliwashukuru watu wote walioshirikina kutoa rai kwa makampuni mbalimbali pamoja na wananchi kuwa tayari kujitolea kwenye shughuli kama hizo wanapotakiwa kufanya hivyo.

“Tunayo furaha kwa mwitikio huu wa kukubali kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu kwa kuonyesha upendo hususan wafanyakazi wa Zantel Zanzibar. Niwaombe muendelee na moyo huu huu wa kujitolea pindi mnapohitajika kushiriki kwenye shughuli nyingine kama hizi,”alisema.

Kwa upande wake, Afisa Uhamasihaji wa Mpango wa damu salama ZanzibarBw. Omar Said Omar alisema kwamba zoezi la uchangiaji damu limefanyika kwa mafanikio makubwa na amefurahishwa na moyo wa kujitolea ulioonyeshwa na wafanyakazi wa Zantel-Zanzibar. Hata hivyo aliongeza kuwa, bado mahitaji ya damu ni makubwa ikilinganishwa na kiwango kilichokusanywa.

Alisema kwamba shughuli ya kukusanya damu ni zoezi endelevu la kujitolea, benki ya damu imekuwa ikiomba makampuni na jamii kwa jumla kutambua umuhimu wa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wananchi.

“Ni watu wachache sana ambao wamekuwa wakijitokeza kuchangia damu, hivyo tunaamini kuwa zoezi hili litaendelea kuwahamasisha watu wengi kujitokeza kushiriki,” alisema.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.