Habari za Punde

Walimu wa mafunzo ya amali washiriki mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo

Na Salmin Juma, Pemba

Walimu wanaosomesha Vituo vya Mafunzo ya Amali  Kisiwani Pemba wametakiwa kuyatumia vyema mafunzo walioyapata ili yaweza kufanikisha malengo yaliokusudiwa.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji kutoka Mamlaka ya Mafunzo  ya Amali Zanzibar Bakari Khamis Juma  wakati alipokwa akifungua mafunzo ya siku tano  huko katika ukumbi wa kituo cha Amali  vitongoji  Chake Chake Pemba.

Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo walimu wa vituo hivyo na kuwa wabunifu  ili nao wakawaendeleze vijana mbinu mbali mbali za kuzalisha miradi itakayopelekea kuapatia  kipato na kuondokana na hali ngumu za maisha.

Aidha  Mkurugenzi  huyo  ameitaka  jamii  kuwapeleka vijana wao waliomaliza masomo ya darasa la kumi  katika vituo vya Elimu Mbadala ili waweze kujiendeleza na shughuli mbali mbali za  ujasiriamali  na kuweza kujiajiri wenyewe.

Kwa  upande wa  wawezeshaji  wa mafunzo hayo wamewataka walimu hao kusikiliza kwa makini mbinu za ubunifu na uvumbuzi wa miradi ili wawe walimu wazuri wanapo wafundisha  vijana namna ya kuzalisha miradi hiyo.

Nao  washiriki wa mafunzo hayo wametowa wito kwa jamii kuwapeleka vijana wao katika vituo hiyvo kwa ajili ya kujiendeleza kitaaluma zaidi  na kujiepusha na  vitendo viovu ndani ya jamii zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.