Na mwandishi wetu
Kufuatia msemo mashuhuri Tanzania wa kua “wanawake wakiwezeshwa wanaweza” hatimae wanawake visiwani Pemba wameibuka kwa kasi katika utendaji kazi mbalimbali ikiwamo katika harakati za kibishara kwa lengo la kukukuza uchumi na kujiongezea kipato.
Hilo limebainika jana huko katika soko la Qatar chakechake Pemba baada ya kuonekana akina mama wakichakarika katika harakati za kibiashara na kuonekana kua kweli wanaweza kutokana na maelezo waliyoyaeleza.
Walipotembelewa na mwandishi wa habari akina mama hao wanaojishughulisha na biashara tofauti ikiwemo ya chakula, uuzaji wa matunda na nyenginezo katika soko hilo wamesema kua hali ya kibiashara inakwenda vizuri na wamejitoa vya kutosha kuhakikisha kipato chao kiuchumi kinakua.
Wamesema kua, ingawa kwa muonekano wa juu juu unaonyesha hali kua nzuri lakini wapo hatarini kupoteza soko la biashara zao kutokana na Baraza la mji chakechake kuwahamisha kuwatoa sehemu moja ya biashara waliyozoeleka kuwapelekwa kwengine hali itakayo waletea usumbufu na hata wateja kwani wanashindwa kufahamu sehemu maalum kwa wajasiriamali hao.
Mmoja ya wafanya biashara sokoni hapo Rehema Said Ali amesema kua, kama wanawake wamejitolea kufanya biashara lakini jambo linalowarudishwa nyuma ni kutokua na kitulizano, hii ni kuondolewa katika sehemu zao za biashara na kupelekwa kwengine kila siku.
Amesema kutokana na hali hiyo imepelekea biashara kua mbaya na wanachokifanya hivi sasa ni kupitisha ada tu kuliko kubakia nyumbani.
Nae Maryam Juma mfanyabiashara wa viungo sokoni hapo amesema kua hali ni ngumu sana kutokana na kuhamishwa kila siku,jitihada wanazifanya ila hazionekani kuzaa matunda.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa baraza la mji wa chakechake Pemba Nassor Suleiman amesema serikali imeshaandaa sehemu maalumu kwa wafanyabiashara wote ambao watakaa hapo kwa utulivu lakini bado mambo machache tu kukamilika.
Amemewataka wafanyabiashara sokoni hapo endapo mambo yakikamilika na wakitakiwa kuhama hapo kuelekea katika soko la Quweit wasikaidi amri hiyo kwani hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakao kwenda kinyume na amri hiyo.
Amesema serikali kupitia baraza la mji linawapenda, kuwajali na kuwathamini wafanyabiashara na wajasiriamali wote na uwamuzi wa kuwahamisha (Qatar) kuwapeleka michakaini (Kuwait) sio kwa lengo la kuwakomoa bali ni kuwajengea mazingira mazuri zaidi ya biashara.
No comments:
Post a Comment