Habari za Punde

Kongamano la Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Zanzibar .

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Dk. Amina Ameir akifungua Kongamano la Siku ya Kiswahili Zanzibar lililoandaliwa na Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) lililofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar na kuhudhuriwa na Wadau wa Lugha ya Kiswahili Zanzibar na kutunukiwa zawadi washindi wa watunzi wa hadithi fupi Zanzibar.
Wasshiriki wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Zanzibar wakifuatilia Kongamano hilo.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Dk Amina Ameir akimkabidhi mshindi wa Utunzi wa Hadithi fupi , Mwanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar Ndg.Omar Gulam Omar.wakati wa Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar. 
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar Dk. Maulid Omar Haji akitowa maelezo ya Kongamano hilo la kuadhimisha Siku ya Kiswahili Zanzibar. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.