Habari za Punde

Ligi Kuu ya Zanzibar Kanda ya Unguja Kati ya Taifa ya Jangombe na JKU Mchezo Uliofanyika Usiku Huu Timu Hizo Zimetoka Sare ya Bila Kufungana

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Jangombe akiwapita wachezaji wa Timu ya JKU wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Kanda ya Unguja uliofanyika Uwanja wa Amaan usiku huu timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana. 
Katika mchezo huo timu zote zimeonesha mpira wa mbele ya mashabiki wao kwa mchezo safi na wa uhakika kila upande umetowa burudani kwa wapenzin wao. Katika mchezo huo timu zote zilikuwa zikitegeana kila moja ikimtegea mwenzake na kupoteza nafasi nyingi za ushinda. 
Kipindi cha pili cha mchezo huo Timu ya JKU ilikuwa ikilishambulia goli la Timu yua Jangiombe lakini mashambulia hayo hayakuleta matunda na kumfanya Kocha wao Mkuu Seif King kutokaa katika benchi na kila mara kusimama na kuwakaripia wachezaji wake.Hadi mwisho wa mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya 0-0

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.