Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mjuwe Dereva wa Teksi Mwanamke Kisiwani Pemba Aishangaza Jamii..

Na Salmin Juma Pemba. 

Leo dunia inaadhimisha Siku ya Mwanamke Duniani, wananchi kisiwani Pemba pia wameungana na wenzawao ulimwenguni kuadhimisha siku hiyo.

Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika leo huko katika ukumbi wa Makonyo chakechake kila aliyehudhuria katika ukumbi huo alionekana kutoamini kwa kile kilichojitokeza lakini iliwabidi waamini kwa kujua huo ndio ukweli ulivyo.

Hali hiyo imejitokeza kufuatia mwanamama aliyejizolea sifa kujitokeza na kunadi kazi yake ya udereva taxi ambapo amesema tokea kuanza kazi yake hiyo sasa anatimiza mwaka mmoja na mambo yanakwenda vizuri.

Dada huyo kwa jina anaitwa Shemsa Hakim Khamis mkaazi wa Chanjamjawiri Pemba, hivi sasa ameshakua dereva anayepata sifa kubwa katika eneo lake la kazi huko uwanja wa ndege Pemba.

Ingawa jamii bado haijamtambua ila sasa wanaanza kumjua, anasema kazi hiyo inamnufaisha vya kutosha na ingawa kuna changamoto za hapa na pale lakini anakabiliana nazo na mambo yanakwenda.

Amezitaja baadhi ya changamoto hizi ikiwamo baadhi ya abiria kutaka kufanya kinyume na maadili ila anaushukuru sana uongozi wa madereva taxi wa uwanja wa ndege chakechake wanaompa sapoti kubwa kwa kuamkinga na mabalaa mbalimbali na mpaka sasa hakuna baya lililomfika.

Katika historia ya zama hizi huyu mama anaandika nambari moja kwa mwanamke Zanzibar kuwa dereva wa taxi tena anaeimudu kazi yake.

Anajivunia kazi yake hiyo huku akitoa wito kwa akina mama wenzake wasijibweteke nyumbani kwani fursa bado zipo ni nyema kuamka na kujikurupusha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.