Habari za Punde

Mke wa Rais wa Tanzania Mama Janeth Magufuli Ahani Msiba wa Sir Georg Kahama Jijini Dar es Salaam.

Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akiweka saini kitabu cha maombolezo baada ya kumfariji  Mama Janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe na Waziri wa Kwanza wa  Ushirika na Masoko katika Baraza la Mawaziri chini ya Serikali ya  Madaraka na baadaye Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Ndani baada ya Uhuru, Marehemu Clement George Kahama maarufu kama  `Sir George Kahama'  aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mama Janeth Kahama, Mama Evelyn Warioba, Anna Kahama-Rupia, Mama Rahma Bomani,Mama Getrude Luangisa, Mama Ishengoma, Mama Feruzi na Mama Tunu Mwapachu.
Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akishiriki katika sala na Mama Janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe Marehemu Clement George  Kahama maarufu kama `Sir George Kahama’ na ndugu, marafiki na jamaa wa familia ya marehemu aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam
Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akimpa pole   Mama janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe na Waziri wa Kwanza wa Ushirika na Masoko katika Baraza la Mawaziri chini ya Serikali ya Madaraka na baadaye Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Ndani baada ya  Uhuru, Marehemu Clement George Kahama maarufu kama `Sir George Kahama' aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam. 
Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akiagana baada ya kumpa pole  Mama Janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe Marehemu Clement George Kahama maarufu kama `Sir George Kahama’ aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Picha na IkuluI.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.