Habari za Punde

Pennyroyal yatoa elimu ya Afya na usafi wa mazingiraKampuni ya Pennyroyal Gibraltar kupitia tawi lake la Best of Zanzibar linalojihususha na shughuli za kusaidia jamii, imeanzisha masomo ya usafi wa mazingira na afya kwa wanajamii wa maeneno ya Kijini and Mbuyu Tende kaskazini mwa kisiwa cha Unguja.

Uhitaji wa elimu hii ulionekana baada ya kufanya utafiti katika vijiji hivyo mwaka jana mwezi Desemba, na kuonekana kuwa kuna changamoto kubwa sana za kiafya katika maeneo hayo ya Unguja Kaskazini. Utafiti ulifanyika na maafisa afya sita kutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) wakisaidiana na kampuni ya Pennyroyal ili kuweza kupata picha na hali halisi ya mahitaji ya vijiji vya Kijini na Mbuyu Tende.  

Baadhi ya matatizo  yaliyogundulika yalikuwa  nipamoja  na elimu finyu ya afya, usafi wamazingira na ukosefu wa vyoo na maji safi.

Masomo haya yatafanyika katika awamu tano, yakianzia kwa viongozi wa jamii wakiwemo masheha na wasaidizi wao, walimu na wanafunzi, kwenye vikundi mbali mbali kama vya akina mama, wavuvi na vijana, na kwenye mahospitali wakati wa kiliniki za kina mama.

Bi Nahya Nassor Khamis, afisa afya alisema ‘Changamoto katika vijiji hivi vya Kijini na Mbuyu Tende niukosefu wa elimu ya afya na usafi wa mazingira ambapo  inachangia kwa kiasi kikubwa kuleta matatizo kwa jamaii ikiwemo magonjwa ya milipuko kwamfano kipindu pindu, maradhi ya ngozi na magonywa ya tumbo.’ 

Bi. Nahya akiwa na maafisa wenzake na wafanyakazi wa Pennyroyal kwenye shule ya Kijini aliendelea kusema, ‘Sasa chini ya usimamisi wa mradi wa Best of Zanzibar na kampuni ya Pennyroyal tunauwezo wakuwasaidia wananchi wa Unguja Kaskazini kubadilisha tabia zao na kujiepusha na maradhi yatokanayo na ukosefu wa elimu ya usafi.’

Bwana Mohamed Issa Khatib msimamizi wa mradi huo toka Best of Zanzibar alisema, ‘Tulipo fanya utafiti mwaka jana  tuligundua asilimia kubwa ya wananchi wa Unguja Kaskazini wanachangamoto mbali mbali zaki maisha. Tumeanza na elimu ya usafi, na kampuni yetu inajitolea kuendelea kuwapa fursa wanawake na vijana wa jamii hizi kupitia masomo ya biashara ili waweze kujiendeleza kimaisha na kupata ujuzi zaidi. 

Tunaamini kwamba kupitia elimu hii ya biashara na ujuzi wakutengeneza bidhaa mbalimbali kama vikapu na sabuni , na mafunzo ya kilimo wananchi wa Kijini na Mbuyu Tende wanaweza kujikwamua kimaisha. Tunaamini kwamba bidhaa hizi zitazotengenezwa na wanajamii hawa zitakuwa kiuvutio kikubwa kw watalii, na wananchi wataweza kuziuza kwa watali hawa na kupitia Zanzibar Amber Resort pale itakapo kamilika na ujenzi.’
Elimu hii itatolewa kwanzia tarehe 27 Februari na awamuya kwanza itakamilika tarehe 9 Marchi 2017.

(Taarifa imetolewa na meneja msimamizi wa Best of Zanzibar Tia Egglestone

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.