Habari za Punde

Ligi Kuu ya Zanzibar Kati ya Timu ya Kilimani Ctry na Chwaka Star Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya Kilimani City Imeshinda Bao 3--0.

Mshambuliaji wa Timu ya Kilimani City kushoto Abdilahih Seif Bausi akizuiya mpira huku beki wa timu ya Chwaka Stars akijaribu kumzuiya wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Kanda ya Unguja mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Timu ya Kilimani City imeshinda mchezo huo kwa mabao 3--0.
Mchezo huo uliokuwa na kila ufundi ukionesha kwa mpizani wake na kuoneshana ufundi wa jinsi ya kucheza mpira. kwa kupeleka mashambulizi kwa zamu.
Timu ya Chwaka Stars itabidi ijilaumu kwa kupoteza mchezo huo kwa kukosa mabao ya wazi kwa kukosa umakini washambuliaji wake hadi mapumziko timu hizo zimekuwa sare ya bila kufungana.
Kipindi cha pili kiliaza kwa mashambulizi ya zamu na kuoneshana jinsi ya kumuliki mpira kwea pande zote. Timu ya Kilimani City imeandaka bao lake la kwanza katika dakika ya 60 ya mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji wake Abdilah Seif Bausi baada ya kumppiga chenga kipa wa timu ya Chwaka aliyeingia kipindi cha pili baada ya kipa wa mwazo kuumia. 
Timu ya Kilimani City imeandika bao lake la pili katika dakika ya 70 ya mchezo huo kupitia kwa mchezaji wake Iddi Farijala  baada ya kuwatoka mabeki wa timu ya chwaka. bao la mwisho kwa timu hiyo limefungwa katika dakika ya 86 ya mchezo huo kupitia kwa mchezaji wake Khelfen Salum. hadi mwisho wa mchezo huo timu ya Kilimani City imetoka kifua mbele kwa mabao 3--0.
 No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.