Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo
kwa Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge kuhakikisha kuwa Mradi wa Maji wa
Ng’apa uliopo mkoani Lindi unakamilika ndani ya miezi mine na si vinginevyo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo
kwa Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge kuhakikisha kuwa Mradi wa Maji wa
Ng’apa uliopo mkoani Lindi unakamilika ndani ya miezi mine na si vinginevyo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mama
Salma Kikwete mara baada ya kuwasalimia wananchi waliokusanyika karibu na mradi
wa Maji wa Ng’apa uliopo Mkoani Lindi. Pia Mama Salma Kikwete amemshukuru Rais
Dkt. Magufuli kwa kumteua kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge mteule Mama Salma Kikwete mara
baada ya kuwasalimia wananchi waliokusanyika karibu na mradi wa Maji wa Ng’apa
uliopo Mkoani Lindi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Ng’apa mara baada ya kutembelea
mradi wa Maji wa eneo hilo ambao unasuasua kukamilika. Rais Dkt. Magufuli
ametoa miezi minne kwa Mkandarasi kampuni ya Overseas Infrastructure Alliance
Private Limited ya India kuhakikisha kuwa inakamilisha ujenzi wa mradi huo na
sio kuleta visingizio.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bodi
ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ikulu ndogo Mkoani
Lindi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara
baada ya kumaliza mazungumzo yake na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika (AfDB) katika Ikulu ndogo Mkoani Lindi. Wakwanza kushoto ni Kiongozi
wa Wakurugenzi hao Lekhethe Mmakgoshi kutoka Nchini Afrika Kusini na Wakwanza
kulia ni Mkurugenzi mwingine wa (AfDB) Dkt.Nyamajeje Weggoro ambaye ni
Mtanzania.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Kiongozi wa Wakurugenzi hao kutoka (AfDB) Lekhethe Mmakgoshi mara baada ya
kumaliza mazungumzo na Bodi hiyo ya Wakurugenzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mmoja wa Wakurugenzi wa (AfDB)
Dkt.Nyamajeje Weggoro mara baada ya kumaliza mazungumzo na Bodi yao Ikulu ndogo
mkoani Lindi.
Sehemu ya Mradi wa Maji wa Ng’apa mkoani
Lindi ambao Rais Dkt. Magufuli ametoa miezi minne kwa mkandarasi anayejenga
mradi huo ili uweze kukamilika haraka.PICHA
NA IKULU
No comments:
Post a Comment