Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dkt Shein afanya mazungumzo na Rais wa jamhuri ya muungano Dkt Magufuli Ikulu Chamwino DodomaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana kwa mazungumzo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatatu Machi 13, 2017. 

Picha na IKULU 
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Dodoma                                        3.3.2017
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli  katika Ikulu ya Chamwino iliyoko mjini Dodoma.

Viongozi hao wawili wamezungumzia mambo mbali mbali kuhusiana na masuala ya kimaendeleo pamoja na kazi kubwa iliyoko mbele yao katika kuleta maendeleo na ustawi wa wananchi wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Dk. Magufuli ameitumia fursa hiyo kumpongeza Dk. Ali Mohamed Shein na kumtakia heri katika siku yake muhimu ya kuzaliwa ambayo ni leo tarehe 13 Machi 2017. Dk. Shein alizaliwa tarehe kama hiyo mwaka 1948 na hivyo kutimiza umri wa miaka 69.

Dk. Shein alisema kuwa ameitumia siku yake hiyo ya kuzaliwa kwa kumtembelea Dk. Magufuli ili waweze kubadilishana mawazo kwani wana kazi kubwa ya kujenga nchi pamoja na kuwaletea maendeleo endelevu wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutumia fursa hiyo kumshukuru Dk. Magufuli kwa kumtakia heri katika siku yake hiyo muhimu ya kuzaliwa.

“Siku ya kuzaliwa  ni siku ya furaha lazima ikumbukwe, lazima isherehekewe, mimi siku yangu ya kuzaliwa sisherehekei sana lakini huwa nafurahi sana na leo nimefurahi sana” amesema Dk. Shein.

Dk. Shein ambaye pia, ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, amerejea Zanzibar leo akitokea Mkoani Dodoma ambako alishiriki vikao mbali mbali vya CCM, ikiwa ni pamoja na Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika hapo jana.

 Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.