Na MatukiodaimaBlog
MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza awataka wananchi mkoani hapa kutowaruhusu wageni kulala na watoto chumba kimoja.
Kuwa kuanzia sasa mgeni akifika nyumbani kwako apewe godoro na kulala sebuleni na sio kushusha watoto vitandani na kumpa heshima mgeni Kulala kitandani chumba cha watoto.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa ushauri huo leo wakati akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Ikanga kata ya Mdabulo wilayani Mufindi ambako maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yalifanyika kwa mkoa wa Iringa.
Alisema kuwa hatua kuwapa vitanda vya ama wageni kuchanganywa chumba kimoja na watoto baadhi yao si wema wapo kwa ajili ya kuwabaka watoto hao"
Pia aliwataka wazazi kutowatuma watoto nyakati za usiku madukani ama nje ya nyumba zao kwani kuendelea kuwatuma watoto hao usiku ni kuwahatarishia usalama wao na wabakaji
Alitaka ikifika usiku wazazi wenyewe mama na baba ndio watumane dukani kama hakuna mtu mzima wa kutumwa na sio mtoto mdogo
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amepongeza taasisi isiyo ya Kiserikali ya RDO inayojishughulisha na huduma mbali mbali za kijamii wilayani Mufindi ikiwemo ya maji na malezi ya yatima.
Pamoja na kuishukuru taasisi hiyo ya RDO chini ya mkurugenzi wake Fidelis Filipatali, bado aliwaonya baadhi ya wanasiasa wanaotaka kukwamisha mradi wa maji kwa kuingiza siasa.
Kuwa mradi huo wa maji hauna siasa na kuwa wananchi wanahitaji maji na sio siasa na kuahidi kuendelea kuwa karibu na asasi hiyo ya RDO.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Marcelina Mkina ambae mjumbe wa NEC Taifa kutoka wilaya ya Mufindi na katibu wa CCM wilaya ya Mufindi walimpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kumteua Masenza kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa na kuwa maendeleo na ushirikiano mkubwa wa serikali na chama umefanikisha maendeleo Kwa wananchi.
Mkini alisema kuwa pongezi za utendaji kazi wa mkuu huyo wa mkoa atazifikisha rasmi kwenye mkutano mkuu wa CCM .
Hata hivyo alipongeza mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanayofanya na serikali ya awamu ya tano pamoja na Vita dhidi ya ufisadi na rushwa na kuwa wao UWT na CCM wapo pamoja na Rais |
No comments:
Post a Comment