Habari za Punde

Skuli ya Alkhamis Camp Yakabidhiwa Vitambu Kwa Ajili ya Skuli Hiyo na Waumini wa Kanisa la Wasabato.

Mwenyekiti wa Kanisa la Wasabato Jimbo la Mashariki na Kati Nchini Tanzania, Ndg.Josheph F.Mngwabi, akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Salama Mbarouk Khatib, msaada wa vitabu kwa ajili ya Skuli ya Alkhamis Camp, inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Pemba.
Mwenyekiti wa kanisa la Wasabato jimbo la Mashariki na kati Tanzania, Joseph F , Mngwabi, akiagana na mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba mara baada ya kumkabidhi vitabu kwa ajili ya Skuli ya Alkhamis Camp Pemba.
Baadhi ya Msaada wa Vitabu , uliotolewa na Kanisa la Wasabato Tanzania kwa Skuli ya Alkhamis Camp, inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)Pemba
Baadhi ya Wanafunzi wa Skuli ya Alkhamis Camp, inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Pemba, wakisikiliza kwa makini hatuba ya mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi Vitabu vilivyotolewa na Kanisa la Wasabato Tanzania .
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Salama Mbarouk Khatib,akimkabidhi Vitabu Mlezi wa Skuli ya Alkhamis Camp inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Pemba, Luteni Kanali Paul Masinde.huko vitongoji Pemba.
                    Baadhi ya Walimu na Wafanyakazi wa Skuli ya Alkhamis Camp Pemba, wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya Vitabu kwa Skuli hiyo vilivyotolewa na Kanisa la Wasabato Tanzania.    Picha na Bakar Mussa-Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.