Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo
ya Nje ya Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu (wakwanza kushoto),
akiongozana na wajumbe wengine wa kamati hiyo baada ya kukagua Mradi wa Ujenzi
wa Ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, iliyofanyika leo jijini Dar es
Salaam.Wa kwanza kulia ni Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Balozi Hassan Simba Yahaya, akijibu baadhi ya hoja zilizoelekezwa na
wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama (hawapo pichani), wakati wajumbe hao
walipotembelea mradi wa ujenzi ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Ziara
hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa jeshi
hilo, Thobias Andengenye
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji, Thobias Andengenye akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa ofisi za jeshi
hilo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na
Usalama(hawapo pichani), wakati wajumbe hao walipotembelea mradi huo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti
wa kamati hiyo, Balozi Adadi Rjabu na anayefuatia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahaya.
Mjumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama,Kapteni Mstaafu George Mkuchika, akichangia
hoja wakati wa ziara ya kamati hiyo kukagua ujenzi wa ofisi za Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji, jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment