STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Pemba 03.04.2017
RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametembelea miradi ya
maendeleo kisiwani Pemba ukiwemo mradi wa barabara, umeme na Chuo cha Mafunzo
ya Amali na kuitaka Kampuni ya ZECON inayojenga Chuo hicho kuhakikisha mradi wa
ujenzi huo unakamilika kwa muda uliopangwa.
Akiwa
katika eneo la chuo hicho huko Daya Mtambwe mara baada ya kupata maelezo kutoka
kwa Kampuni ya Ujenzi pamoja na Mshauri Mwelekezi alisisitiza kuwa mradi huo ni
wa Serikali na Wizara ya Elimu ni wasimamizi tu, hivyo alieleza umuhimu wa
kumalizika mapema mradi huo kwa maslahi ya wananchi.
Alieleza
kuwa changamoto za kiufundi zilizojitokeza katika kutekeleza mradi huo hazina
budi kupatiwa ufumbuzi wa haraka ili utekelezaji wa mradi huo uweze kukamilika
kama ilivyopangwa.
Mara
baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Chuo cha Amali kilichopo Daya Mtambwe, Dk.
Shein alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi pamoja na wanafunzi wa Skuli ya
Msingi Daya katika viwanja vya skuli hiyo na kusisitiza lengo la Serikali la kujenga
chuo hicho.
Dk.
Shein alisema kuwa ujenzi wa Chuo hicho utawasaidia wale wanafunzi waliokuwa
hawakupata fursa ya kuendelea na masomo ya juu na kuweza kupata mafunzo ya
vitendo yakiwemo mafunzo ya kiufundi.
Alisema
kuwa uwamuzi wa Serikali ni kujenga chuo hicho kama kilivyo chuo cha Amali cha
Vitongoji kwa upande wa Pemba na Mkokotoni Unguja na kusisitiza kuwa ujenzi huo
utakwenda sambamba na ujenzi wa chuo cha Amali huko Makunduchi.
Aidha,
Dk. Shein alisema kuwa ujenzi wa Chuo hicho ni ahadi aliyoitoa wakati wa Kampeni
za uchaguzi mkuu uliopita wakati akiwahutubia wananchi huko Kangagani, na
kusisitiza utekelezaji wa ahadi yake hiyo upo pale pale.
Alisema
kuwa licha ya ujenzi huo kusita kutokana na sababu za kiufundi kwa takriban
miezi saba kwa hivi sasa na kueleza kuwa si zaidi ya wiki tatu ujenzi huo
utaendelea na matarajio ni kumalizika hapo mwakani.
Mapema
Dk. Shein alipata fursa ya kukagua ukarabati wa barabara ya Chwale (Madenjani)
hadi Mzambarautakao wenye urefu wa kilomita 5 unaoendelea kwa kiwango cha lami
ambao unatarajiwa kumalizika baada ya wiki moja.
Mkuu
wa Mradi kutoka Kampuni ya MECCO, Crispin Prosper Mwombeki, alimueleza Dk.
Shein kuwa ukarabati huo baada ya miezi saba umefanywa kwa muda wa miezi mitatu
ili kwenda na hali halisi ya jiografia ya Pemba.
Pamoja
na hayo, Mwombeki alieleza changamoto zilizopo hasa katika suala zima la utaratibu
wa upatikanaji wa kifusi kwa ujenzi wa barabara huku akieleza haja ya kuweko na
utaratibu wa kudumu wa ukarabati wa barabara hizo ndani ya mwaka mmoja.
Wakati
huo huo, Dk. Shein alifika Ukunjwi kwa ajili ya kuangalia mradi wa umeme
unaopelekwa katika kisiwa cha Fundo.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment