Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Kutoka Dar hadi Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi mikoa ya Kigoma na Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia majina ya baadhi ya wataalamu mbalimbali waliohusika katika mchakato wa Ujenzi huo wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza. Wakwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa akiwa ameshika majina hayo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akichota mchanga na kuweka kama ishara ya kushiriki katika ujenzi huo wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kibao cha jiwe la msingi cha Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa, Mama Janeth Magufuli wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Masanja Kadogosa wakati akielezea kuhusu ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amechuchumaa kwenye mfano wa Reli ya Kisasa (SGR) na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Masanja Kadogosa, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu Profesa Norman Sigala mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli hiyo, wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na  Hawa Ghasia (Mb) 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa wakati akipita katika katika ya mfano wa Reli hiyo itakayojengwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kaimu Mtendaji Mkuu wa RAHCO Masanja Kadogosa wakati akielekea kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa Reli hiyo ya Kisasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa Reli hiyo ya Kisasa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe Abubakary Zubeiry mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika eneo la Pugu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza msanii Mrisho Mpoto mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi huo wa Reli ya Kisasa Pugu jijini Dar es Salaam. 
Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.