Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya
UKIMWI kwa Kaimu KatibuTawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Wambura Sabora (hayupo pichani)
wakati Mkurugenzi Mkuu huyo wa NBS alipofanya ziara mkoani humo hivi karibuni kuangalia jinsi zoezi
la utafiti huo linavyoendelea.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt.
Albina Chuwa (kulia) akiwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Wambura Sabora wakati Mkurugenzi Mkuu huyo wa
NBS alipofanya ziara mkoani humo hivi karibuni kuangalia jinsi zoezi la Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya
UKIMWI linavyoendelea.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS) Dkt. Albina Chuwa (katikati) akiwa na Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Kituo
cha Kukinga na Kuzuia Magonjwa (CDC) Dkt. Eunice Mmari (kulia) wakipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa wadadisi wanaofanya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya
UKIMWI Bw. John mark Obura wakati wa ziara iliyofanyika mkoani Kagera hivi karibuni kuangalia jinsi zoezi
la utafiti huo linavyoendelea.
Mdadisi Bi. Shinuna
Said akichukua damu kwa mmoja wa wakazi wa kijiji cha
Chonyonyo wilaya ya Karagwe mkoani Kagera hivi karibuni kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya
UKIMWI unaofanyika nchi nzima.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa
(kulia) akiwa na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la ICAP Tanzania Dkt. Fernando Morales
(katikati) pamoja na Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkaazi wa Kituo cha
Kukinga na Kuzuia Magonjwa Tanzania (CDC) Dkt. Eunice Mmari (kushoto) wakiangalia jinsi Mdadisi
Bi. Shinuna Said (hayupo pichani) anavyochukua damu kutoka kwa mmoja wa wakazi wa kijiji
cha
Chonyonyo wilaya ya Karagwe mkoani Kagera hivi karibuni kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI wakati wa ziara iliyofanyika mkoani humo kuangalia jinsi zoezi
la utafiti huo linavyoendelea.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS) Dkt. Albina Chuwa akimuhoji mmoja wa wakazi wa kijiji cha
Chonyonyo wilaya ya Karagwe mkoani Kagera kuhusu jinsi zoezi la
Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI
lilivyofanyika katika kaya yake.Mahojiano hayo yamefanyika wakati Mkurugenzi Mkuu huyo wa
NBS alipofanya ziara mkoani humo hivi karibuni kuangalia jinsi zoezi la
utafiti huo linavyoendelea.
Mdadisi Bw.
John mark Obura akihojiwa na baadhi ya waandishi wa habari kuhusu jinsi zoezi la
Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI linavyofanyika mkoani Kagera wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS) Dkt. Albina Chuwa iliyofanyika hivi karibuni kuangalia jinsi zoezi la
utafiti huo linavyoendelea.
Na: Veronica
Kazimoto.Bukoba
Imeelezwa kuwa asilimia 97 ya watanzania wanaoishi katika kaya
zilizochaguliwa kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI katika
mikoa 11 ambayo imeshafikiwa hadi sasa, wameshiriki kikamilifu katika utafiti huo unaoendelea
kufanyika nchini.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa utafiti
huo kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Wambura Sabora alipofanya ziara
mkoani humo kuangalia jinsi zoezi la utafiti huo linavyoendelea.
"Ninayo furaha kukutaarifu kwamba,mpaka sasa utafiti huu umeshafanyika
katika mikoa 11ya Tanzania Bara pamoja na visiwa vyote vya Zanzibar yaani Pemba
na Unguja. Jambo la kufurahisha zaidi ni mwitikio wa wananchi ambao ni asilimia
97 ya wanaoishi katika kaya zilizochaguliwa kwa ajili ya utafiti kukubali
kushiriki," amesema Dkt. Chuwa.
Mikoa ambayo imekamilisha utafiti huu wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI ni
pamoja na Singida, Dodoma, Manyara, Iringa, Njombe na Ruvuma. Mikoa mingine ni
Mbeya, Songwe, Katavi, Tabora na Kigoma.
Nae Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Wambura Sabora amemwambia
Mkurugenzi Mkuu wa NBS kwamba, zoezi la utafiti huo mkoani humo linaendelea
vizuri na mpaka sasa hakuna tatizo lolote lililoripotiwa ofisisini kwake.
"Nami nichukue fursa hii kukueleza kwamba zoezi hili linaendelea
vizuri hapa mkoani Kagera na mpaka sasa hakuna shida yoyote iliyojitokeza.
Aidha, maeneo ya Kerwa, Missenyi na Wilaya ya Bukoba tayari yamekamilisha
utafiti huu", amesema Sabora.
Kwa upande wake mmoja wa wakazi wa
kijiji cha Chonyonyo wilaya ya Karagwe mkoani Kagera aliyehojiwa na Mkurugenzi
Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa kuhusu jinsi alivyoshiriki kwenye utafiti huo, alisema amefurahishwa na utafiti huo kwa kuwa amepata
fursa ya kupima vipimo mbalimbali ambavyo hakutarajia kuvipata vyote kwa wakati
mmoja.
"Kwakweli nimefurahishwa na utafiti huu kwakuwa sikutarajia kupima
vipimo vya magonjwa ya Homa ya Ini, Kaswende pamoja na UKIMWI kwa wakati mmoja
nikiwa nyumbani kwangu," ameeleza Mkazi huyo wa kijiji cha Chonyonyo.
Utafiti huu wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania unaendeshwa na Ofisi
ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Tanzania Bara, Wizara ya Afya kwa Tanzania
Zanzibar, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar (OCGS), Tume ya Taifa ya
Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) na Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC).
No comments:
Post a Comment