Habari za Punde

Amour Janja atokea benchi na kupeleka msiba Jang'ombe Boys

Timu ya kikosi cha JKU iliyoifunga Jan'gombe Boys


Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Ligi kuu ya Zanzibar hatua ya 8 bora jioni ya leo imemaliza mzunguko wa 3 kwenye dimba la Amaan ambapo Timu ya JKU imefanikiwa kutoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Jang’ombe Boys.

Mchezo huo ambao ulikuwa mgumu kwa timu zote mbili na kupelekea hadi mapumzika hakuna timu iliyoona lango la mwenziwe.

Kurudi kumaliza kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko kwa kila upande kutaka kuondoka na alama tatu muhimu lakini mchezaji aliyetokea benchi Amour Omar “Janja” akaipatia alama tatu JKU baada ya kufunga bao katika dakika ya 89 ya mchezo.

Ligi hiyo itakwenda mapumziko kupisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kisha kuendelea mzunguko wa nne ambapo mpaka sasa Jamhuri ndie kinara mwenye alama 9 kufuatia kushinda michezo yake yote mitatu ya awali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.