Habari za Punde

Mkutano wa Sita wa Baraza la Wawakilishi Kuanza Mei 10 2017.

Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Bi Raya Issa Msellem akizungumza na waandishi swa habari kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya Mkutano huo wa Baraza unaotarajiwa kufanyika jumatano ya wiki hii. na kuleza kumla ya muswali 182 yataulizwa na kupatiwa majibu kupitia mkutano huo. 

Pia amesema kutakuwa na kuwasilishwa Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa Mwaka Fedha 2017/2018.

Na kuwasilishwa Miswada ya Sheria itawasilishwa na kujibiwa miswada yenyeweni kama ifuatayo.
 i. Mswada wa Sheria ya Fedha (Finance Bill)

ii. Mswada wa Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018.

iii. Mswada wa Sheria ya (Marekebisho) ya Sheria ya Maadali ya Viongozi wa Umma Nam.4. ya mwaka 2015.

Miswada ya Dharura
iv. Mswada wac Sheria ya Kufuta Sheria ya Ushuru wa Stempu (Stamp Duty)
v. Mswada wa Sheria ya Ushuru wa Bidhaa (Excise Duty)

 Amesema kutawasilishwa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mwaka 2014/2015. Na kuwasilishwa Taarifa za Serikali kuhusu Utekelezaji wa Hajo.
i).Taarifa ya Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Hoja za Baraza la Wawakilishi kuhusiana na Uingizaji na Utumiaji wa Madawa ya Kulevya Zanzibar

ii).Taarifa ya Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto kuhusu utekelezaji wa Maazimio ya Hoja ya Baraza la Wawakilishi kuhusiana na Uimarishaji wa mfumo mzima wa kisheria na uendeshaji wa kesi za udhalilishaji wa Wanawake na Watoto.
    

Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Raya Issa Msellem akisisitizajambo wakati akijibu mswali ya waandishi wa habari katika mkutano wa kutowa Taarifa ya kuanza kwa Mkutano wa Sita wa Baraza wiki hii. 
Waandishi wakiwa makini wakifuatilia taarifa hiyo ikitolewa na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Raya Issa Msellem katika ukumbi mdogo wa baraza Chukwani Zanzibar.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.