Habari za Punde

Mwandishi wa Bomba FM apata bonge la Shavu, achaguliwa kuwa Afisa habari kamati ya soka la ufukweniNa: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Suleiman Ussi Haji “Mido” ambae ni muandishi na mtayarishaji wa kipindi cha michezo cha SPORTS BOMBA cha Bomba FM amechaguliwa kuwa afisa Habari wa Kamati ya Soka Ufukweni visiwani Zanzibar.

Mara baada ya Chama cha Soka Visiwani Zanzibar kupata uanachama wa kudumu wa 55 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” wakaitaka Kamati ya soka la ufukweni kuunda uongozi mpya ambao sasa rasmi kwasasa umewekwa hadharani.

Uongozi huo ambao unaongozwa na Ali Sharifu “Adolf” ambae ni Mwenyekiti, Katibu Fahad Khamis, mshika fedha Hassan Ali Mzee, mjumbe Ali Omar Abdallah huku Muhsin Ali “Kamara” na Mohd Rajab ni washauri wa kamati hiyo ambapo Afisa Habari ni Suleiman Ussi Haji “Mido” .

Tayari kamati hiyo imeshapata baraka zote kutoka ZFA taifa na imepania kuanza rasmi majukumu yake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.