WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO
YA AMALI ZANZIBAR INATANGAZA NAFASI ZA MASOMO SHAHADA YA KWANZA NA YA PILI
NCHINI MISRI KATIKA CHUO CHA “AL-AZHAR” KWA MWAKA WA MASOMO 2017/18.
SIFA ZA MUOMBAJI
SHAHADA YA PILI
· Awe
Mzanzibari.
· Awe
amemaliza Shahada ya kwanza
· Awe
na afya nzuri
· Awe
hajajiunga na chuo chengine.
SHAHADA YA KWANZA
· Awe
mzanzibari.
· Awe
amemaliza kidato cha sita au Stashahada.
· Awe
na afya nzuri.
· Awe
hajajiunga na chuo chengine.
NJIA YA KUFANYA MAOMBI
Waombaji wote wanatakiwa
kuwasilisha maombi yao Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar,
wakiambatanisha vitu vifuatavyo:-
·
Kivuli cha kitambulisho cha Mzanzibari
·
Vivuli vya vyeti vya masomo
·
Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
·
Kivuli cha pasi ya kusafiria
·
Fomu ya uchunguzi wa afya.(medical report)
FANI ZINAZOTOLEWA Ni za Art
na Science
NJIA YA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yatumwe kwa
anuani ifuatayo:-
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Amali, S.L.P 394 Zanzibar.
IMPITIE
Mkuu wa Kitengo Cha uratibu
Elimu ya Juu, Sayansi na Teknologia, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,
Zanzibar.
Lugha itakayotumika katika
masomo hayo ni lugha ya Kiarabu
Kwa maelezo zaidi fika
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mazizini chumba namba 57
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI HAYO
NI TAREHE 1/6/2017
No comments:
Post a Comment