Habari za Punde

Akutwa tayari ameshafariki shambani kwake


Na. Salama Nassor - Pemba.

MTU mmoja, aliyejulikana kwa jina la Kombo Mohamed Ali (Dileji (42) ambae alikuwa fundi gereji mkaazi wa Chanjamjawiri Chake Chake Pemba, ameokotwa akiwa amefariki Dunia huko Shambani kwake Jumbe ,Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Kamanda Sheikhan Mohamed Shekhan, amesema leo majira ya saa 2-15, asubuhi amepokea tarifa  ya kuonekana maiti kwenye la shamba ya marehemu huyo huko Jumbe Chanjamjawiri Wilaya Chake Chake.


“Ni kweli ameokotwa maiti ili katika eneo hilo kwa muda wa siku tatu, katika hatua ya mwazo wa upelelezi umebaini marehemu alitoweka nyumbani kwake kwenda shambani kwa shughuli zake za kilimo.akiwa anaumwa, lakini hata  nilipofika eneo la tukio nikaona Jembe na inaoneka aliwahi kulima kidogo”,alisema Kamanda Shekhani.

Akitowa wito kwa jamii kuwa na utamaduni wa kutowa tarifa katika vyomba   husika pindipo wanapopotelewa na ndugu zao ili kuweza kujuwa matatizo yaliyomkumba.


Kwa upande wa Dokta dhamana wa Hospitali ya Chake Chake, Sharifu Hamad Khtib, alisema kifo cha marehemu kilikuwa cha kawaida baada ya kumpima na wala alikuwa hana alama ya aina yoyote ambayo ilimdhuzu.


Mwili wa marehemu teyari umeshakabidhiwa  kwa familia yake kwa ajili ya mazishi baada ya uchunguzi wa Daktari.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.