Habari za Punde

Raza Lee awapiga Tafu mabingwa watetezi wa Rolling Stone

RAZA LEE AWAPA TAFU MABINGWA  WATETEZI WA ROLLING STONE


Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.

Mwana michezo Mohd Ibrahim “Raza Lee” ambae ni mtoto wa Mbunge wa Jimbo la Kiemba Samaki Ibrahim Raza asubuhi ya leo ameisaidia mipira timu ya kombaini ya Mjini Unguja ambao ni Mabingwa  watetezi wa Mashindano ya Vijana ya Rolling Stone, Mashindano ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi June 29, 2017 na kumalizika July 9, 2017 jijini Arusha.

Mipira hiyo Raza Lee ameikabidhi timu hiyo Dukani kwake ambalo ni Duka la Vifaa vya Michezo ambapo Ali Othman “Kibichwa” Meneja wa Timu hiyo pamoja na Mohammed Seif “King” kocha wa timu hiyo ndio waliyopokea Mipira hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.