Habari za Punde

Serikali yapokea msaada wa saruji na mchele kwa ajili ya wananchi waliopatwa na maafa ya mvua za masika

 Meneja wa Kampuni ya Hawaii Clearing and Fowarding Bwana Thabit Maalim Kulia akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Paketi za Mchele Tani Moja na Nusu kwa ajili ya Wananchi walioathirika na Mvua za Masika.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia akipokea Saruji Paket 1,000 kutoka kwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Evergreen Limited Bwana Abdughafur Ismail kwa ajili ya Wananchi walioathirika na Mvua za Masika hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Balozi Seif akiyashukuru Makampuni yaliyojitokeza kusaidia Waathirika wa Mavua za Masika baada ya kupokea Msaada wa Mchele na Saruji kutoka kwa Kampuni ya Evergreen Limited na Hawaii Clearing and Fowarding.

Picha na OMPR


Na Othman Khamis


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  imepokea msaada wa  Paketi  1,000 za Saruji kutoka kwa Kampuni  ya Evergreen Limited na Tani moja na nusu za mchele kutoka kwa Kampuni ya Hawaii Clearing and Forwading  kwa ajili ya kusaidia Wananchi waliopatwa na maafa ya mafuriko ya Mvua za Masika zinazokaribia ukiongoni mwake.

Msaada huo umepokelewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi seif Ali Iddi ulioshuhudiwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed na maafisa watendaji wa Ofisi hiyo hapo Vuga Mjini Zanzibar.

Bwana Abdulghafar Ismail Meneja Mkuu wa Kampuni ya Evergreen Lilited alikabidhi saruji hiyo kwa niaba ya Kampuni yenye thamani ya shilingi Milioni 14,000,000/- na Bwana Thabit Maalim Meneja wa Kampuni ya Hawaii Clearing and Fowarding akakabidhi msaada wa mchele kwa niaba ya Taassi yake wenye Thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni Moja na Nusu.

Wawakilishi hao wa Kampuni hizo za Kibiashara Zanzibar  walisema wameamua kutoa misaada hiyo wakiitikia wito wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kuwataka Wananchi, Wafanyabiashara na Wahisani kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwasaidia Wananchi waliokumbwa na Maafa ya mvua za Masika.

Walisema maafa waliyoyapata Wananchi hao katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Unguja na Pemba yameleta fadhaa na kuwafanya kukosa muelekeo wa kuanza upya kwa harakati zao za kimaisha kiasi kwamba hali hiyo wanastahiki kupata msukumo utakaowapa matmaini mapya.

Akipokea msaada huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  aliushukuru Uongozi wa Kampuni ya Evergreen Limited na ule wa Hawaii Clearing and Fowarding  kwa imani ulioonyesha wa kusaidia waathirika wa Mafuriko ya Mvua za Masika.

Balozi Seif alisema Wananchi wote waliokumbwa na mafuriko hayo katika maeneo tofauti Unguja na Pemba wanastahiki kupata msaada  na wale walioguswa na tukio hilo wanapaswa kuwaonea huruma waathirika hao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Viongozi wa Kampuni hizo kwamba msaada waliotoa  utawafikia walengwa katika kipindi kifupi ili uwasaidiae kuondokana na shida zinazowakabili kipindi hichi kigumu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.