Habari za Punde

Serikali inathamini mchango mkubwa unaotolewa na Serikali ya Cuba hasa katika Sekta ya Afya na Elimu

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar {SUZA} kutoka Nchini Cuba hapo kwenye makaai yao Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Aliyempa Mkono ni Dr. Luis Alfonso, wa kwanza kutoka Kulia ni Dr. Dr. Maria Del Carmen na kulia ya Dr. Alfonso ni Dr. Rosario Maria Acosta.
 Balozi Seif Kulia akibadilishana mawazo na Wahadhiri wa Suza kutoka Nchini Cuba.
 Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar {SUZA} kutoka Nchini Cuba wakiwa makini kufuatilia mazungumzo ya Balozi Seif hapo kwenye makaazi ya Mbweni.

 Mkuu wa Timu ya Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha SUZA kutoka Cuba Dr. Luis Alfonso akiwasilisha salamu zao za shukrani kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Seif.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  amewatembelea Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar {SUZAZ} kutoka Nchini  Cuba  hapo kwenye Makaazi yao Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Balozi Seif  amewaahidi Wahadhiri hao  kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini mchango unaotolewa na Serikali ya Cuba hasa katika Sekta ya Afya na Elimu kwa kuleta Wahadhiri  wanaofundisha Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar {SUZA}.

Aliwahakikishia Wahadhiri hao wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar {SUZA} kutoka Nchini Cuba kuishi kwa Amani na Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi itazingatia maisha yao bila ya wasi wasi wowote.

Balozi Seif  alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikifanya jitihada za kutafuta wataalamu wa Kigeni kusaidia fani tofauti za ujuzi Nchini ili kuwapa faraja wananchi wake kuweza kukabiliana na harakati zao za kimaisha za kila siku.

Naye Mkuu wa Timu ya Wahadhiri hao wa Cuba Dr. Luis Alfonso kwa niaba ya Wahadhiri wenzake ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuvishukuru vyombo vya ulinzi kwa hatua za haraka zilizochukuliwa katika kuwapa ulinzi wa uhakika Wahadhiri hao.

Timu ya Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar { SUZA } kutoka Nchini Cuba wameanza kusomesha Chuo hicho kwa utaratibu wa Miaka Mitatu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.