Na Mwandishi wetu
WAZIRI wa Afya
mhe. Mahmoud Thabit Kombo amefanya
ziara ya kushtukiza katika hospitali kuu ya Mnazimmoja na kukuta kasoro mbali
mbali za kiutendaji ikiwemo walinzi wanaolinda hospitalini hapo baadhi yao hawapo
katika sehemu zao za kazi na walinzi wengine wakiwatolea lugha zisizoridhisha
baadhi ya watu waliofika hospitalini hapo.
Ziara hiyo alioifanya
usiku wa kuamkia leo ambapo aliweza kutembelea wodi vitengo mbali mbali
na kuwakuta wafanyakazi wakiwa katika sehemu zao wakiwahudumia wagonjwa licha
ya kuwepo kwa upungufu wa wafanyakazi baadhi
ya wodi.
Kutokana hali hiyo
ameuagiza Uongozi wa Hosptali hiyo kuchukua hatua stahiki katika kukabilina na
matatizo mbali mbali yanayojitokeza ikiwemo suala la walinzi wanaolinda
hospitalini hapo kwa lengo la kuwapatia
wananchi huduma bora za afya.
Alifahamisha ziara yake hiyo imeweza kubaini changamoto za
wafanyakazi zikiwemo upungufu wa wafanyakazi ambapo ameahidi kulitafutia
ufumbuzi suala hilo haraka iwezekanavyo
ili kuweza kufanikisha utendaji wa kazi katika hospitali hiyo ambayo ndio
kimbilio la wananchi .
Katika ziara yake hiyo Mheshimiwa Mahamoud ameweza kutembelea
sehemu mbali mbali ikiwemo wodi ya wazazi, sehemu ya upasuaji, kitengo cha
huduma za dharura, wodi za wagonjwa Mahatuti, wodi zote za wanaume na wanawake
pamoja na sehemu ya X ray na kuwakuta wafanyakazi wakiwa katika sehemu zao
wakiendelea kuwahudumia wagonjwa.
Alifahamisha kuwa ziara hizo za kushtukiza katika Hospitali
kuu ya Mnazimmoja na hosptali nyengine
zote za Unguja na Pemba zitakuwa
endelevu kwa lengo la kuwabaini wafanyakazi ambao watakiuka maadili ya kazi zao
na kuwachukulia hatua ili kuepuka malalamiko kwa wananchi.
Ziara hiyo ya Waziri
wa Afya katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja imekuja kufuatia hoja mbali mbali za
wajumbe wa baraza la wawakilishi zilizoibuka katika baraza hilo na Waziri wa
Afya kuahidi kuzifanyia kazi.
kuwa inatokana na ahadi yake Mhe. Waziri wa Afya ya kushuka chini Ngazi ya Utendaji ili kuhakikisha ufanisi, Uwajibikaji na Usimamizi na kuwataka Watendaji wote waungane nae mkono badala ya kulalamika kuwa wanaingiliwa katika majukumu Yao.
Majukumu yote ya Wizara ya Afya na Hospitali pamoja na Vituo vyake vyote Vya Afya vipo chini ya Dhamana ya Wizara Ya Afya ambapo yeye Waziri wa Afya ndiye aliye na Dhamana Kuu ya Wizara hiyo katika Usimamizi na Utendaji ulio bora katika kutoa Huduma kwa Wananchi wote ww Zanzibar bila ya Ubaguzi wa Aina yoyote.
Pia Mhe. Waziri wa Afya ametoa tamko la kushirikisha Kitengo cha Huduma kwa Jamii na Ustawi Wa Jamii kushirikishwa kikamilifu pale panapokuwa na tatizo ama upungufu wa Huduma au Mawasiliano kwa Wagonjwa na Wauguzi wanaotokana na Familia zao." .
No comments:
Post a Comment