Habari za Punde

Waziri wa Fedha akiwasili Katika Viwanja Vya Baraza Kuwasilisha Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Hii ndio Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.Ndivyo inavyoonekana akisema Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk Khalid Salum.
Gari iliomchukuwa Waziri Fedha na Mipango Zanzibar Mhe Dk Khalid Salum ikiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar nje kidogo ya Mji wa Unguja.Wilaya ya Magharibi B' Unguja kuwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. 
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dk.Khalid Salum akiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar kuwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 akiinua juu Mkoba ulobeba Bajeti hiyo kwa waandishi wa habari leo asubuhi akielekea katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi kuwasilisha kwa Wajumbe wa Baraza kuisoma na kuchangiwa.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk Khalid Salum akiwa na Moba wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 akiwasili katika viwanja hivyo.
Waziri wa Fedha Zanzibar Dk Khalid Salum akiingia katika jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk Khalid Salum akiwa na tabasamu wakati akiingia katika jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar kuwasilisha Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Khalid Salum Waziri wa Afya Mhe Mahmoud Thabit Kombo na Mwakilishi wa Chaani Zanzibar Mhe Nadir Abdul-Latif na Mwakilishi wa Chukwani Zanzibar Mhe Mwanaasha wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumpokea Waziri wa Fedha alipowasili katika jengo la Baraza.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk Khalid Salum akiingia katika yukumbi wa Mkutano wa Sita wa Baraza la Wawakilishi kuwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018, kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dk.Khalid Salum akiwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza la Sita la Wawakilishi akiwa na Mkoba uliobeba Bajeti Kuu ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa Mwaka 2017/2018 tayari kwa kuisoma na kuiwakilisha kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuichangia. Wajumbe wa Baraza wakimshangilia wakati akiingia katika ukumbi huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.