Habari za Punde

Askarii vyuo vya mafunzo watakiwa kujiepusha na migogoro

Na Salmin Juma, Pemba

ASKARI wa vyuo vya Mafunzo Kisiwani  Pemba wametakiwa kujiepusha na migogoro, majungu na Fitna na kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi ili kulinda nidhamu na heshima jeshi hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba  Mhe Omar Khamis Othman amesema kuwa majungu na fitna  ni sumu sehemu za kazi na kuwasisitiza askari hao kujengeana heshima miongoni mwao.

Katika hotuba yake ya Kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Vyuo vya Mafunzo Pemba, Haji Hamoud Haji iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Abied Juma Ali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa amesema ili kuleta ufanisi wa kazi ni budi askari kufuata maadili ya kazi yao .

Amesema kuwa iko haja kwa Askari wa Vyuo Vya Mafunzo kufufua utamaduni wa kufanya kazi kwa kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya Nchi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea na ubabaishaji .

kwa upande wake Naibu Kamishna wa Vyuo vya Mafunzo Zanzibar Haji Hamoud Haji  ameahidi kuendelea kushirikiana na askari wa Vyuo vya Mafunzo Kisiwani Pemba na atafanya kazi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wote .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.