Habari za Punde

Mwakilishi Tumbe kulikoni kuwakimbia wananchi?

Na Mwandishi wetu

BAADA ya kuvumilia kwa muda mrefu wananchi wa Jimbo la Tumbe wakifikiria kwamba  huenda mwakilishi wao waliyemtuma kuwawakilisha kwenye Baraza la Wawakilishi ataweza kushirikiana nao katika kuwatatulia kero na changamoto zinazowakabili .

Wamesema kwa kipindi chote hicho wananchi hao wamekuwa wavumilivu hatimaye wameshindwa kujizuia na kutoa malalamiko lakini bado jitihada hizo hazijazaa matunda.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wamesema kiongozi muajibikaji ni yule ambae huwa tayari kushirikiana na wananchi wake ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabli sambamba na kutathmini maendeleo yaliyopo .

 Wameeleza kwamba kitendo cha kuwakimbia wananchi baada ya lengo la kupatiwa kura kukamilika sio suluhisho bora kwa kiongozi mwenye kujali maslahi kwa wananchi waliomchagua.

Hali hiyo ni tofauti kwa mwakilishi wa jimbo la Tumbe Ali Khamis Doholo ambae amelalamikiwa na wananchi wa jimbo hilo kwa kukwepa kutekeleza majukumu yake ambayo aliyaahidi kabla ya kuchaguliwa

“Awali tulikuwa na matumaini kwaba tumepata kiongozi ambae ataweza kuzitatua kero zetu kutokana na ahadi alizozitoa wakati wa kampeni lakini baada ya kuchaguliwa tu kiongozi huyo amegeuka kakakuona ndani ya jimbo haonekani wala hasaidii shuhuli za maendeleo ”alisema.

Aidha waandishi wa habari walipofanya jitihada ya kumtafuta kwa njia ya simu kutaka maelezo hakuwa tayari kutoa ushirikiano akidai akiwa tayari atawatafuta.

Mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Tumbe amekuwa na kawaida ya kuwakwepa wandishi wa habari wanapohitaji kupata maelezo juu ya malalamiko ya wananchi waliomchagua jambo ambalo linakwamisha kupatikana taarifa za maendeleo katika Jimbo hilo .

“Mimi binafsi nimekuwa nikisumbuka sana kumtafuta Mwakilishi wa huyo , lakini juhudi zangu zimeshindwa kuzaa matunda baada ya kuendelea kupigwa danadana ”alisema mmoja wa wandishi wa Habari .

Wananchi hao wamemuomba naibu Katibu Mkuu wa CCM Abdallah Juma Mabodi kufanya ziara ya kikazi katika Jimbo ili kusaidia kuhoji utekelezaji wa ahadi za mwakilishi alizozitoa wakati akiomba kura .

Wamesema kitendo cha Naibu Katibu Mkuu wa CCM kufanya ziara katika jimbo hilo kunamfanya Mwakilishi wao aone aibu kutokana na kitendo chake cha kuwakimbia wapiga kura wake

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.